Mchekeshaji Erick Omondi akamatwa akiongoza maandamano Kisumu

Maandamano hayo yalikuwa yakifanyika kando ya barabara za Jomo Kenyatta

Muhtasari

•Waandamanaji walilalia magodoro na kufunga barabara ya Jomo Kenyatta, hali iliyowalazimu polisi kutumia vitoa machozi.

•Mapema mwezi hii, Eric alikamatwa wakati akiandamana dhidi ya gharama ya juu ya maisha na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Central.

alikamatwa akiongoza maandamano mjini Kisumu Aprili 26, 2023
Eric Omondi alikamatwa akiongoza maandamano mjini Kisumu Aprili 26, 2023
Image: FAITH MATET

Mchekeshaji Eric Omondi amekamatwa mjini Kisumu.

Omondi alikuwa akiongoza baadhi ya wakazi katika maandamano ya kupinga gharama ya juu ya maisha, kuongezwa kwa ada na ukosefu wa ajira. Maandamano hayo yalikuwa yakifanyika kando ya barabara za Jomo Kenyatta

Waandamanaji walilalia magodoro na kufunga barabara ya Jomo Kenyatta, hali iliyowalazimu polisi kutumia vitoa machozi.

OCPD wa Kisumu ya Kati Nicholas Maina amethibitisha kukamatwa kwa Omondi katika jiji hilo  la kando ya ziwa.

alikamatwa akiongoza maandamano mjini Kisumu Aprili 26, 2023
Mchekeshaji Erick Omondi alikamatwa akiongoza maandamano mjini Kisumu Aprili 26, 2023
Image: FAITH MATETE

Haya yanajiri takriban wiki tatu baada ya mchekeshaji huyo kukamatwa tena akiandamana jijini Nairobi.

Mapema mwezi hii, Eric alikamatwa wakati akiandamana dhidi ya gharama ya juu ya maisha na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Central.

Baadaye, mchekeshaji huyo asiyepungukiwa na drama alifikishwa mahakamani ili kujibu shtaka la kusababisha fujo jijini Nairobi.

Ilidaiwa kuwa mnamo Aprili 3, mwendo wa saa tano unusu mchana, kwenye barabara ya Kenyatta Avenue, alizua fujo kwa njia ambayo huenda ikasababisha uvunjifu wa amani kwa kuweka kizuizi katikati ya barabara.

Polisi walisema baada ya kuweka kizuizi hicho katikati ya barabara, alikipanda na kuanza kupiga kelele na kusababisha fujo. Kizuizi hicho kilisababisha vikwazo na kuwasumbua watumiaji wengine wa barabara.

Omondi alidaiwa kutenda kosa hilo mnamo Aprili 3, 2023, kando ya Barabara ya Kenyatta ndani ya jiji la Nairobi.

Hata hivyo, alikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Zainabu Abdul na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh5,000 pesa taslimu.

Wakili wake Danstan Omari alikuwa ameiomba mahakama kumpa mshtakiwa masharti nafuu ya dhamana.

"Waheshimiwa, nakusihi umpatie mteja wangu masharti nafuu ya bondi ili aweze kuendelea na kazi yake ya kutengeneza maudhui mtandaoni," Omari alisema.

Kesi hiyo ilitajwa tena Aprili 13 kwa ajili ya kusikilizwa mapema.