Rais Museveni awataka Waturkana wa Kenya kuwakabidhi wenzao waliohusika na mauaji ya Wanaakiolojia

Museveni aliwaonya raia wa Turkana kwamba jamii yao ambayo kwa sasa inaishi Uganda itafukuzwa.

Muhtasari

• Mwezi Aprili mahakama ya kijeshi katika mkoa wa Karamoja iliwafunga jela Wakenya 30 hadi miaka 20 kwa kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Image: BBC

Rais wa Uganda,Yoweri Museveni amewataka Waturkana wa Kenya kuwakabidhi waliohusika na mauaji ya wanajiolojia watatu katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo mwezi Machi mwaka jana kwa ajili kufikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi.

Katika agizo hilo la rais Museveni lililotolewa wiki moja iliyopita lakini lilitangazwa hadharani Jumatano hii, Museveni aliwaonya raia wa Turkana kwamba jamii yao ambayo kwa sasa inaishi Uganda itafukuzwa na watu wao kutoruhusiwa kuvuka mpaka na kuingia katika mkoa wa Karamoja ili kuwalisha wanyama wao iwapo watashindwa kufanya hivyo.

Museveni hata hivyo alisema watuhumiwa wanaweza kushirikiana na serikali ya Kenya na Uganda kuchagua mfumo wa jadi wa haki wa fidia kwa waathirika.

Wana miezi sita ya kutekeleza matakwa ya Rais.Iwapo Turkana itaamua kulipa fidia,Museveni anasema ni lazima iendane na mchango ambao marehemu angeweza kutoa katika maisha yao ya kazi.

Pia watalazimika kuwapa jamii ya Jie zaidi ya ng’ombe 2000 waliopotea wakati wa uvamizi wa ng'ombe.

Kabla ya tarehe ya mwisho,Museveni pia alitoa amri ya ziada kwa vyombo vya usalama kumkamata Mturkana yeyote anayeingia nchini kinyume cha sheria kwa bunduki na kuwafungulia mashitaka ya ugaidi.

Mwezi Aprili mwaka huu mahakama ya kijeshi katika mkoa wa Karamoja iliwafunga jela Wakenya 30 hadi miaka 20 kwa kumiliki silaha kinyume cha sheria na risasi baada ya kukamatwa wakati wa zoezi la kusalimisha silaha.

Kuendea kwa bunduki haramu mipakani ikiwa ni pamoja na Uganda, Kenya na Sudan Kusini katika miaka ya hivi karibuni kumesababisha kuongezeka kwa wizi wa mifugo.

Athari zake kwa jamii zilizoathirika zimekuwa mbaya, na kuwaacha wakiwa wakiwa katika mkwamo wa umasikini.