Watu wavutiwa na Ardhi inayotetemeka Njoro, Nakuru

Sehemu hiyo yaweza kuwa kivutio cha wataii na kigezo cha ushuru wa Kaunti

Muhtasari

•miaka hamsini iliyopita pahali  hapa palikuwa kidimbwi, baadaye pakakauka na ndiposa nyasi zikamea juu yake kufanya nji kavu.

•Kwa baadhi ya wakaaji mtetemeko huu unaleta msisimko ila kwa wengine unafurahisha kwa jinsi unavyotepetea huku wengine wakihofia kuzama.

Ardhi tepetevu
Ardhi tepetevu

Wodi ya kihingo, Njoro kaunti ya Nakuru, imkuwa kivutio kwa wakaaji na hata watalii kutokana na asili ya kipekee yenye Ardhi ambayo hutetemeka mtu anapotembea au kurukaruka juu yake.

Wakaaji wa eneo hilo wamtoa maoni tofuti tofauti wengo wakidai kuwa ardhi hiyo inaweza kutengwa na kuhifadhiwa kama sehemu ya utalii.

Kutokana na hali hiyo ya kutetemeka wakaaji walipaita maali hapo "Kinaini"

Robert Maina mkaaji wa eneo hilo anaeleza kuwa,miaka hamsini iliyopita pahali  hapa palikuwa kidimbwi, baadaye pakakauka na ndiposa nyasi zikamea juu yake kufanya nji kavu.

Ila panasemekana kuwa n maji chini ya ardhi hiyo jambo ambalo hufanya sehemu hiyo kutetemeka.

Kwa baadhi ya wakaaji mtetemeko huu unaleta msisimko ila kwa wengine unafurahisha kwa jinsi unavyotepetea huku wengine wakihofia kuzama.

Hata hivyo wamegundua sehmu hii na kuifadhi kuwa sehmu ya utalii kwa watu wanaotmbelea Kaunti hiyo.

Japo utafiti wa kina hujafanywa kubaini kiini cha utepetevu huo, wakaaji sasa wanadai kuna haja ya kutenga sehemu hiyo kuwa ya utalii jambo ambalo wanasema litapelekea kaunti hiyo kunawiri  kwa kupata kipato kikubwa cha ukusanyaji wa ushuru.

Kulingana na Kennedy Barasa, ambaye ni katibu wizara ya Raslimali,kuna uwezekano sehemu hiyo kuwa na mgama  ambayo ni mawe yanayoyeyuka na kuwa kama uji ndiposa ukitembea unahisi kwamba unatembea juu ya maji.

aida Katibu huyo ameeleza kuwa kuna haja ya kutenga sehemu hiyo kuwa kivutio cha utalii.

"Hiyo inaweza kuw kitega cha uchumi kwa wakaaji na inaweza kuleta ushuru kwa Kaunti,"

Utafiti unaonyesha kuwa Barani Afrika kuna Ardhi eneo la duara nchini Cameroon ambayo inayumba na kuwa ya kwanza Barani Afrik.

Kaunti ya Kiambu pia ina kidimbwi ambacho huyumbayumba mtu anapotembea na kinatambuliwa kuwa cha pili Afrika.