logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Gavana wa Meru Kawira Mwangaza akamatwa

Ripoti za zilionyesha kuwa programu hiyo ilikuwa imepigwa marufuku hapo awali na Serikali

image
na Davis Ojiambo

Habari18 October 2023 - 12:20

Muhtasari


  • • Mwangaza alikamatwa baada ya kujaribu kufanya programu ya okolea jamii katika eneo la Ruiga ya Kati huko Imenti.
Gavana wa kaunti ya Meru Kawira Mwangaza akamatwa baada ya kujaribu kufanya kipindi cha Okolea eneo la Ruiga ya Kati Picha Dennis Dibondo

Gavana wa Meru Kawira Mwangaza amekamatwa. Mwangaza alikamatwa alipokuwa akiendesha mpango wa Okolea katika eneo la Ruiga ya Kati huko Imenti.

Katika taarifa yake baada ya kukamatwa, Gavana Mwangaza alithibitisha kuwa kweli yuko mikononi mwa polisi. 

Hata hivyo alilaumu mamlaka kwa kushindwa kuendelea na hatua zinazofuata za taratibu za kisheria baada ya kukamatwa kwake. Kulingana na Gavana, maafisa hao wa polisi 'wamemzuilia' kwenye gari la polisi.

"Niko chini ya ulinzi. Maafisa wa polisi hawataki kunipeleka Kituo ili kufungua mastaka. Wamenishikiliwa kwenye gari hili la polisi kwa saa mbili sasa," alisema.

 "Inasikitisha kuona juhudi za kulemaza harakati za kuleta maendeleo ambazo zinakusudiwa kusaidia masikini katika jamii yetu vitisho kama hivyo visiruhusiwe kutatiza maendeleo katika jamii ya Wameru," aliongeza.

Gavana huyo alisema maafisa wa polisi walitumwa kutatiza utekelezaji wa mpango huo.Awali gavana huyo alikuwa ametangaza kwamba angesambaza ng'ombe kwa familia zenye mahitaji, chini ya mpango wa Okolea.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved