•Siku ya Jumanne, mahakama ya Shanzu ilitupilia mbali faili ya kesi dhidi ya Mchungaji Odero baada ya miezi kadhaa ya kusikilizwa.
•"Faili za uchunguzi kuhusiana na Bw Odero unaendelea na hakuna kesi dhidi yake iliyokatishwa inavyodaiwa,” Ingonga alisema.
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Renson Ingonga sasa anasema kwamba kesi dhidi ya Mchungaji Ezekiel Odero haijafungwa, jinsi ilivyokuwa imeripotiwa kote.
Kwa mujibu wa Ingonga, kuna uchunguzi unaoendelea kuhusu suala hilo, huku akisisitiza kuwa Hakimu Mkuu Joe Omido alifunga tu faili ya mahakama katika kesi hiyo, kinyume na ripoti zilizotajwa kwamba kesi ya Ezekiel imetupiliwa mbali.
"Tungependa kufafanua kuwa uhakiki kwamba faili za uchunguzi kuhusiana na Bw Odero unaendelea na hakuna kesi dhidi yake iliyokatishwa inavyodaiwa,” Ingonga alisema.
Alibainisha kuwa uchunguzi utakapokamilika, ataamua hatua inayofuata huku akisema ODPP itafanya uamuzi kuhusu matokeo ya uchunguzi punde tu uhakiki wake utakapokamilika, DPP alisema.
Baada ya kupokea faili za uchunguzi, ODPP aliridhika kwamba maagizo ya mahakama ya kuwezesha uchunguzi tayari yametimiza madhumuni yao na haikuwa lazima kwa Odero kuendelea kuhudhuria korti au kituo cha polisi.
Siku ya Jumanne, mahakama ya Shanzu ilitupilia mbali faili ya kesi dhidi ya Mchungaji Odero baada ya miezi kadhaa ya kusikilizwa na kuagiza arudishwe dhamana yake ya Sh 1.5m pesa taslimu.
Mahakama ilisikiza kwamba Mchungaji Ezekiel anachunguzwa kwa tuhuma za mauaji, utekaji nyara, itikadi kali, mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya binadamu, ukatili wa watoto, utapeli.