Matokeo ya KCPE na KPSEA yatatolewa kabla ya Krismasi, asema katibu Belio Kipsang

Watahiniwa milioni 1.4 walifanya mitihani yao ya KCPE na takriban milioni 1.2 wakifanya mitihani ya KPSEA

Muhtasari

•Kundi la mwaka huu lilikuwa la mwisho kufanya KCPE ili kuandaa njia ya utekelezaji kamili wa Mtaala Unaozingatia Umahiri (CBC) katika shule za msingi ambao sasa utashuhudia wanafunzi wakifanya mitihani ya KPSEA

Katibu wa Idara ya Elimu ya Msingi Belio Kipsang azungumza na Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu

Katibu wa kudumu wa elimu Belio Kipsang ametangaza kuwa watahiniwa waliofanya mitihani ya Cheti cha Elimu ya Msingi ya Kenya (KCPE) na Elimu ya Shule ya Msingi ya Kenya (KPSEA) watapokea matokeo yao kabla ya  sherehe za Krismasi.

Alisema haya siku ya Jumatano alipokuwa akitoa taarifa kuhusu zoezi la mtihani wa kitaifa, ambapo washikadau wanaohusika kwa kunafanyika zoezi hilo.

Kipsang alisisitiza kuwa zoezi la kuweka alama linaanza mara moja na  kupewa kipaumbele kuhakikisha zoezi la kusahihisha linakamilika kwa muda unaofaa.

"Yote yamekwenda sawa,Ningependa kuwashukuru walimu wetu kwanza kwa kazi nzuri, wenzetu kutoka TSC, timu za usalama, na timu zingine zote ambazo zimefanya kazi nasi," alisema.

Jumla ya watahiniwa milioni 2.6 walikuwa wakifanya mitihani hiyo katibu Kipsang alisisitiza kuwa wizara itahakikisha kwamba hakuna mtu atakayeachwa nje katika kipindi cha mpito hadi ngazi inayofuata ya elimu.

Takriban watahiniwa milioni 1.4 walifanya mitihani yao ya KCPE na takriban milioni 1.2 walifanya mitihani ya KPSEA (Daraja la 6).

"Mwaka huu tulikuwa na idadi ndogo ya wajawazito, uwezeshaji tunaowapa wazazi wetu unazaa matunda.

Tunafurahi kwamba tunapunguza tishio hili la mimba za utotoni," alisema akitathmini kesi zilizotengwa wakati wa mzunguko wa mitihani wa 2023.

Kundi la mwaka huu lilikuwa la mwisho kufanya KCPE ili kuandaa njia ya utekelezaji kamili wa Mtaala Unaozingatia Umahiri (CBC) katika shule za msingi ambao sasa utashuhudia wanafunzi wakifanya mitihani ya KPSEA.