Je? maoni yako ni yapi baada ya SGR kuongeza nauli kwa wasafiri kwenda Pwani?

SGR imepandisha nauli zake kwa asilimia 50 kwa wasafiri wake

Muhtasari

• Bei hizo ziliorodheshwa upya kwa Huduma ya abiria ya Madaraka Express, Huduma ya Reli ya Nairobi Commuter, Treni ya Safari ya Kisumu na Treni ya Safari ya Nanyuki.

Mradi wa reli ya SGR ulifadhiliwa na serikali ya CHINA

Ni pigo kwa wasafiri wanaojiandaa kwa shamrashamra za musimu wa krismasi mwaka huu baada shirika la reli la kisasa SGR kutangaza kutoza nauli za juu kwa yeyote anayetaka kupata huduma za usafiri kupitia shirika hili.

Wakenya wengi hupendelea huduma za shirika  hili la reli ya kisasa kwa jinsi ambavyo ilitoza nauli za chini kwa usafiri  ila kwa sasa  nauli katika  maeneo yote inayopeana huduma zake za usafiri imepadisha kwa asilimia 50.

Katika hakiki ya hivi punde, abiria wa Mombasa sasa watalipa Sh1,500 kuanzia Januari 1, 2024, kutoka Sh1,000  nauli hii ikiwa imepanda kwa shilingi mia tano.

Kwa  wasafiri  wale wanaotaka kusafiri na daraja la kwanza, watalazimika kulipa Sh4,500, kutoka Sh3,000 nauli hii ikipadishwa kwa shiliingi elfu moja mia tano.

Hata hivyo shirika hili limebainisha kuwa tikiti zilizonunuliwa kabla ya wakati huo, hata hivyo, hazitaathirika.

Nauli  ya wasafiri kutoka Kibwezi hadi Mombasa itagharimu Sh890 huku Voi hadi Mombasa ikigharimu Sh440.

Bei hizo ziliorodheshwa upya kwa Huduma ya abiria ya Madaraka Express, Huduma ya Reli ya Nairobi Commuter, Treni ya Safari ya Kisumu na Treni ya Safari ya Nanyuki.