Polisi waanzisha msako kumtafuta mgemaji wa pombe haramu - Murang`a

Hii ni baada ya lita 680 za chang`aa inayoaminika kuwa ya mshukiwa kukamatwa katika msako wa polisi Jumatano usiku.

Muhtasari

• Akizungumza na vyombo vya habari siku ya Alhamisi, Kamishna wa Kaunti ya Murang’a Patrick Mukuri alisema pombe hiyo ambayo inakadiriwa kuwa na thamani ya Sh500,000 ilizuiliwa baada ya polisi kupokea ripoti

• “Tunaendelea na mapambano hayo na tuntoa  onyo kali kwa wanaoendelea kutengeneza pombe hiyo, tunataka kuwaambia wanahatarisha maisha ya watu

vyombo vinavyotumiwa kubebea pombe haramu
vyombo vinavyotumiwa kubebea pombe haramu

Polisi huko Murang’a wameanzisha msako wa kumsaka mshukiwa mkuu wa utengenezaji na usambazaji wa pombe haramu katika kaunti ndogo ya Kahuro.

Mshukiwa ambaye polisi walisema anajulikana sana anayesemekana kuwa na viunga 19 vya pombe ndani ya kaunti moja pekee.

Hii ni baada ya lita 680 za chang`aa inayoaminika kuwa ya mshukiwa kukamatwa katika msako wa polisi Jumatano usiku.

Akizungumza na vyombo vya habari siku ya Alhamisi, Kamishna wa Kaunti ya Murang’a Patrick Mukuri alisema pombe hiyo ambayo inakadiriwa kuwa na thamani ya Sh500,000 ilizuiliwa baada ya polisi kupokea ripoti kutoka kwa umma kuhusu shehena hiyo.

Aidha Mukuri aliwaonya wale ambao bado wanajihusisha na utengenezaji wa pombe haramu katika kaunti hiyo kuwa serikali itawajia.

“Tunaendelea na mapambano hayo na tuntoa  onyo kali kwa wanaoendelea kutengeneza pombe hiyo, tunataka kuwaambia wanahatarisha maisha ya watu wetu na sisi kama serikali hatutakubali jambo hili liendelee. ,” Mukuri alisema.

Kamanda wa polisi kaunti ya Murang’a David Mathiu kwa upande wake amesema polisi wamekuwa wakimsaka mshukiwa ambaye ameendelea kuweka maisha ya wakenya hatarini.

Alisema biashara hiyo haramu ya pombe imesababisha vijana wengi wa eneo hilo kukosa manufaa kwani wengi wao huanza kunywa asubuhi kutokana na kuwapo kwa pombe hizo.

“Tumekuwa tukimtafuta mshukiwa mmoja ambaye ameunganishwa na shehena hiyo iliyozuiliwa jana usiku. Mshukiwa ameweka maisha ya Wakenya wengi hatarini,” Mathiu alisema.

Mathiu aliongeza kuwa maisha ya vijana yanazidi kudidimia kwa sababu ya uwepo wa pombe hiyo ambayo inauzwa kwa bei nafuu katika maenoe tofauti ambayo wauzaji wametenga.

"Vijana wengi hawawezi kupanga taratibu za siku yao kwa sababu asubuhi wanapata pombe ya bei nafuu kutoka kwa viungo ambavyo anafanya kazi. Kwa mfanomshukiwa  ana viungo karibu 19 ndani ya Kitongoji kimoja; kwa hivyo unaweza kutathmin madhara ambayo watu wa eneo hili wanakumbana nayo ,” aliongeza.