Naibu Rais Rigathi akutana na familia ya narehemu msanii Ally B

Rigathi Gachagua apeana pole yake kwa familia ya Ally B,huku akiaidi kuwasaidia kimaisha

Muhtasari

•Naibu wa Rais aliandamana  mwanasiasa na mwanamuziki Jaguar

Gachagua akutana na familia ya Ally B
Gachagua akutana na familia ya Ally B
Image: X

Naibu wa Rais Rigathi Gachagua mapema leo ameshapisha taarifa  kwenye mtandao wake wa X akiwa  pamoja na  familia ya aliyekuwa msanii Ally B ambaye alifariki siku chache zilizopita.

Kulingana na naibu wa rais msanii huyo alikuwa maarufu kwa utunzi wa nyimbo huku akisema kuwa Ally B alichangia sana katika uchanguzi wa mwaka 2022 kwa ushawishi wake kwa vijana wa pwani.

 "Leo asubuhi katika Makazi Rasmi hapa Mombasa, niliikaribisha familia ya marehemu Mwanamuziki Ali Mwakaribu Ally B, aliyefariki mapema mwezi huu kwa ajili ya kuwafariji na kuwatia moyo,...

Ally B aliinuka kutoka katika hali ya unyonge alipiga hatua ya kitaifa kwa nyota yake ya muziki, ambao ulimfafanua kama mtu binafsi mwenye kipaji cha kipekee,Pia namkubuka kwa usaidizi wake usioyumba wakati wa kampeni zetu za uchaguzi,"ulisoma ujumbe wa Rigathi.

Naibu wa rais  Pia alichapisha  ujumbe maalum kutoka kwa Rais Ruto amboa alisema alitumwa na Rais.

"Natuma faraja yangu  tunapoendelea kuombea Roho ya Ally B ipumzike kwa Amani ya Milele, tutatembea maisha haya pamoja na familia yake changa,tasnia ya Sanaa ya Ubunifu ni msingi wa Utawala wangu  tunapotafuta kukuza vipaji vinavyowezekana, sio tu kwa burudani na kuelimisha,"ulisema ujumbe wa Rais.

Naibu wa Rais aliandamana  mwanasiasa na mwanamuziki Jaguar.