Vatican yathibitisha marufuku ya Wakatoliki kuwa Freemasons

Vatican imethibitisha marufuku iliyopo kwa waumini wa kanisa katoliki kuwa wanachama wa muungano wa Freemasons.

Muhtasari

• Wiki iliyopita Vatican ilisema kwamba watu waliobadili jinsia wanaweza kubatizwa na kuwa mashahidi kwenye harusi za Wakatoliki.

Kiongozi wa kanisa katoliki papa Francis
Kiongozi wa kanisa katoliki papa Francis

Vatican imethibitisha marufuku iliyopo kwa waumini wa kanisa katoliki kuwa wanachama wa muungano wa Freemasons.

Waraka mpya uliotiwa saini na Papa Francis umesema mafundisho ya Kikatoliki na uanachama wa Freemason hayawezi kutangamana au hayapatani .

Barua hiyo iliyotolewa na ofisi ya mafundisho ya Vatikani ilinukuu tamko lililotolewa miaka arobaini iliyopita, likisema kwamba wakatoliki waliojiunga na chama cha freemason hawaruhusiwi kushiriki katika ekaristi takatifu.

Uamuzi huo wa hivi karibuni unaonekana kumjibu Askofu kutoka Ufilipino ambaye alionyesha wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa idadi ya Wakatoliki katika dayosisi yake wanaojiunga na vyama vya freemason.

Ofisi hiyo hiyo ilisema wiki iliyopita kwamba watu waliobadili jinsia wanaweza kubatizwa na kuwa mashahidi kwenye harusi za Wakatoliki.

Barua hiyo kuhusu Freemasons ilinukuu tamko la mwaka 1983, lililotiwa saini na Papa Benedict XVI, wakati huo mkuu wa mafundisho ya Vatikani, likisema kwamba Wakatoliki "katika vyama vya Kimasoni wako katika hali ya dhambi kubwa na huenda wasipate Ushirika Mtakatifu