NSSF yatangaza nafasi zaidi ya 300 za kazi

Watu wanaovutiwa wanashauriwa kuwasilisha wasifu kazi katika makao ya azina hiyo kabla ya tarehe 11 Desemba 2023.

Muhtasari

• Katika notisi, kuna nafasi 336 ambazo hazina hiyo inataka watu wenye kutuma maombi ya kazi

• “Hazina ya Kitaifa ya malipo ya uzeeni ina vituo vya kutolea huduma vilivyoenea kote nchini na inalenga kuimarisha uwezo wa rasilimali  ili kutimiza wajibu wake wa kutoa huduma kwa Wakenya wote,”

Image: HISANI

Hazina ya kitaifa ya malipo ya uzeeni NSSF imetangaza nafasi za kazi katika sekta mbalimbali.

Katika notisi, kuna nafasi 336 ambazo hazina hiyo inataka watu wenye kutuma maombi ya kazi.

“Hazina ya Kitaifa ya malipo ya uzeeni ina vituo vya kutolea huduma vilivyoenea kote nchini na inalenga kuimarisha uwezo wa rasilimali  ili kutimiza wajibu wake wa kutoa huduma kwa Wakenya wote,” ilisema notisi hiyo.

Baadhi ya nafasi hizo ni pamoja na meneja wa Mkoa (6), meneja msaidizi (19), meneja wa tawi (15), afisa mkuu mwandamizi (28) mhasibu (24), afisa  wa usalama (2),msimamizi wa rekodi (2), afisa mkuu (78). ) msimamizi mkuu wa wakufunzi (46) miongoni mwa nafasi nyinginezo.

Watu wanaovutiwa wanashauriwa kuwasilisha wasifu kazi katika makao ya azina hiyo kabla ya tarehe 11 Desemba 2023.

Takwimu kutoka kwa ripoti ya Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya ya Ripoti ya Wafanyakazi wa Kila Robo ya Oktoba-Desemba 2022 ambayo ilitolewa Februari inaonyesha ukosefu wa ajira nchini Kenya ulipungua hadi 960,001 ambayo ni  (asilimia 4.9) katika kipindi cha Desemba 2022 kutoka 1,055,816 ambayo ni  (asilimia 5.6) katika robo hiyo hiyo  ya mwaka wa 2021.

Serikali imesema itatoa nafasi za kazi kwa vijana.

Wiki iliyopita, Waziri wa Utumishi wa Umma na Usimamizi wa Uwasilishaji Moses Kuria alisema wizara yake hivi karibuni itazindua tovuti ya 'Jobo Bila Connection initiative'.

Waziri huyo alisema tovuti hiyo itawasaidia Wakenya kutuma maombi ya kazi katika sekta ya umma bila kujali asili zao.

"Katika sekta ya umma, tutaongoza kutoka mbele. Hivi karibuni tutatengeneza tovuti ya Wakenya wote kutuma maombi ya kazi katika sekta ya umma bila kujali asili yao iliyopewa jina la Jobo Bila Connection initiative," alisema.

"Suala la ukosefu wa ajira kwa vijana linapaswa kuwa wasiwasi kwetu sote kwa sababu hatuko salama hadi pale sisi sote tutakuwa salama" alisema.