Wanaharakati wampa heko CS Kindiki kwa juhudi za kukabili ujambazi

Wanaharakati hao sasa wanamtaka waziri kuendelea na vita dhidi ya ujambazi na changamoto zingine za ukosefu wa usalama kote nchini.

Muhtasari

• Wawakilishi wa mashirika ya kiraia wakiongozwa na Kipkorir Ngetich walisema kuwa Kindiki amejitolea kwa nadra katika kazi yake ya kuongoza  vita dhidi ya ujambazi 

• "Kwa mara ya kwanza, tuna waziri ambaye yuko mikononi mwake na anamaanisha kile anachosema,"

Waziri wa usalama na maswala ya ndani Kithure Kindiki
Waziri wa usalama na maswala ya ndani Kithure Kindiki
Image: HISANI

Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki amepata sifa kutoka kwa wanaharakati wa eneo la Kaskazini kwa juhudi zake za kumaliza ujambazi na changamoto zingine za usalama kote nchini.

Wawakilishi wa mashirika ya kiraia wakiongozwa na Kipkorir Ngetich walisema kuwa Kindiki amejitolea kwa nadra katika kazi yake ya kuongoza  vita dhidi ya ujambazi hasa  katika eneo la Kaskazini.

"Kwa mara ya kwanza, tuna waziri ambaye yuko mikononi mwake na anamaanisha kile anachosema," Ngetich alisema.

Alisifia utendakazi wa Kindiki akisema kuwa ni mara ya kwanza kulingana na yeye kuwa na waziri ambaye anaonoza kwa msitari wa mbele katika kupambana na waalifu.

"Waziri alisema atapiga kambi Kerio Valley kusaidia kukabiliana na ujambazi na hatujawahi kuwa na waziri mwingine yeyote wa usalama ambaye amekuwa katika eneo hilo zaidi yake."

Ngetich ambaye anaongoza Kituo cha Haki za Kibinadamu na Demokrasia alisema mashirika ya kiraia yanayohudumu katika eneo laKaskazini yamerekodi kupungua kwa visa vya mashambulio ya ujambazi huko Pokot Magharibi, Baringo, Elgeyo Marakwet, Turkana na Samburu miongoni mwa maeneo mengine.

Maoni yake yaliungwa mkono na wanaharakati wa haki za binadamu Kibet Maswai na Pauline Suter.

 Wanaharakati hao sasa wanamtaka waziri  kuendelea na vita dhidi ya ujambazi na changamoto zingine za ukosefu wa usalama kote nchini.

Ngetich alitaja ukadiriaji wa wapiga kura kuwa wa kweli ambao ulimweka Kindiki kama waziri aliyefanya vyema zaidi katika serikali ya Kenya Kwanza.

Alisema Waziri huyo pia amefanya vyema katika kukabiliana na mashambulio ya kijambazi na akawataka Wakenya kumpa usaidizi anaohitaji katika kubadilisha vyombo vya usalama ili vihudumiwe vyema na kuwezeshwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Kindiki amesifiwa kwa kufanya kazi ya kuboresha sheria na masharti ya huduma kwa maafisa wa usalama ili kuwapa motisha.

"Tumeona Kindiki akifikia hatua ya kukutana na maafisa wa usalama waliotumwa katika eneo hili ili aweze kuelewa changamoto zinazowakabili na kuwapa usaidizi wanaohitaji kufaulu," Ngetich alisema.

Magavana kutoka eneo hilo wakiongozwa na Wesley Rotich wa Elgeyo Marakwet pia wamempongeza Kindiki kwa kujitolea kwake bila kuyumbayumba kuhakikisha wakazi wa eneo hilo wanafurahia amani baada ya miaka mingi ya mashambulizi ya mara kwa mara na mabaya ya ujambazi.