logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Matokea ya mtihani wa KPSEA kuchelewa kutolewa

Njeng'ere aliangazia kuwa uwekaji alama unaendelea na matokeo yatatolewa kabla ya kuendelea na Shule ya Sekondari ya msingi.

image
na Davis Ojiambo

Habari23 November 2023 - 08:09

Muhtasari


  • •Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza la Kitaifa la Mitihani la Kenya David Njeng'ere mnamo Alhamisi alitangaza kwamba usahihishaji bado unaendelea 
  • •Jumla ya watahiniwa 1,282,574 walisajiliwa na kufanya mitihani ya  KPSEA mwaka huu.

Wanafunzi waliofanya mitihani yao ya Tathmini ya Elimu ya Shule ya Msingi ya Kenya (KPSEA) watalazimika kusubiri kwa muda majibu ya mitihani hiyo.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza la Kitaifa la Mitihani la Kenya David Njeng'ere mnamo Alhamisi alitangaza kwamba usahihishaji bado unaendelea kwani walilazimika kutanguliza mitihani ya  KCPE.

"Kwa wazazi na walezi ambao watoto wao walikalia mitihani ya  KPSEA, fahamu tu kwamba tulipaswa kutanguliza matokeo ya KCPE ili  kuafikia taratibu za jinsi wanafunzi hao watakapojiunga na kidato cha kwanza  kabla ya sherehe za Krisimasi," alisema.

Jumla ya watahiniwa 1,282,574 walisajiliwa na kufanya mtihani wa  KPSEA mwaka huu.

Njeng'ere aliangazia kuwa uwekaji alama unaendelea na matokeo yatatolewa kabla ya kuendelea na Shule ya Sekondari ya msingi(Junior school).

Alibainisha kuwa matokeo yatatolewa katika ripoti tatu; ya kila mwanafunzi, ripoti mahususi za shule na ripoti ya kitaifa ya tathmini ya msingi shuleni na muhtasari wa mitihani hiyo.

Ripoti ya kitaifa itaangazia maeneo yanayohitaji usaidizi pamoja na idadi ya wanafunzi katika kila kiwango cha ufaulu kwa kila mada inayohitaji usaidizi.

Ripoti ya shule ya kibinafsi itaundwa kulingana na kila shule na itaangazia maeneo ambayo wanafunzi wanakabiliwa na matatizo na ambapo shule zinahitaji usaidizi zaidi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved