Vijana wasiokuwa na kazi pia kulipia bima mpya ya afya (SHIF)

Serikali imesema kwamba mpango huo mpya utawapa Wakenya wote fursa ya kupata huduma za afya kwa bei nafuu, bila kujali hali yao ya ajira.

Muhtasari

• Wafanyakazi katika sekta rasmi, ya umma na ya kibinafsi, watahitajika kutoa mchango wa kila mwezi wa 2.75% ya mshahara wao wa jumla.  

Waziri wa Afya Susan Nakhumicha
Waziri wa Afya Susan Nakhumicha
Image: MAKTABA

Kila mkenya wakiwemo vijana ambao bado hawajapata kazi wenye umri wa zaidi ya miaka 25 watalazimika kulipa bima mpya ya afya ya Jamii (SHIF).  

Kulingana na tangazo la wizara ya afya vijana wa Kenya wasio na ajira hawatasazwa katika mchango mpya wa kila mwezi wa Hazina ya Bima ya Afya ya Jamii (SHIF) kuanzia tarehe 1 Julai 2024. 

Serikali imesema kwamba mpango huo mpya utawapa Wakenya wote fursa ya kupata huduma za afya kwa bei nafuu, bila kujali hali yao ya ajira. 

Waziri wa Afya Susan Nakhumicha alisema mchango wa kila mwezi katika mpango huo utakuwa wa lazima kwa Wakenya wote walio na umri wa zaidi ya miaka 25. Wafanyakazi katika sekta rasmi, ya umma na ya kibinafsi, watahitajika kutoa mchango wa kila mwezi wa 2.75% ya mshahara wao wa jumla.  

Wakenya wanaofanya kazi katika sekta rasmi watashirikiana na KSh 300 kila mwezi kuelekea mpango huo. Hata hivyo, CS Nakhumicha alisisitiza kwamba wale ambao hawajaajiriwa na walio na umri wa zaidi ya miaka 25 watalazimika kulipa mchango wa KSh 300.  

"Kutokana na rekodi tulizo nazo kutoka NHIF iliyopita, walioajiriwa ni takribani familia milioni 3 kati ya jumla ya kaya milioni 5.5." 

Kulingana na waziri Nahumicha ni vijana walio chini ya miaka 25 pekee ndio watafurahia manufaa ya wazazi wao.