Polisi watafuta genge lililomuua mzee 54 mtaani Korogocho

Mwili wa Peter Njuguna ulipatikana kwenye dimbwi la damu muda mfupi baada ya kudungwa kisu kifuani na watu wasiojulikana.

Muhtasari

• Sababu ya tukio hilo haikuweza kufahamika mara moja.

• Polisi wanasema washambuliaji walitoroka eneo la tukio kabla ya mwili wa Njuguna kugunduliwa.

Mwili
Mwili
Image: HISANI

Mwanamume mwenye umri wa miaka 54 alidungwa kisu na kuuawa katika shambulio la kundi la watu katika mtaa wa Korogocho, Nairobi.

Mwili wa Peter Njuguna ulipatikana kwenye dimbwi la damu muda mfupi baada ya kudungwa kisu kifuani na watu wasiojulikana.

Walioshuhudia waliambia polisi kuwa marehemu alikuwa akipigana na takriban watu watano ndipo alipodungwa kisu na kuuawa.

Sababu ya tukio hilo haikuweza kufahamika mara moja. Polisi wanasema washambuliaji walitoroka eneo la tukio kabla ya mwili wa Njuguna kugunduliwa.

Mwili wake ulikuwa na jeraha kubwa la kisu kwenye bega la kushoto na ulihamishwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri uchunguzi wa maiti.

Wakati huo huo, mlinzi alifariki baada ya kulalamikia matatizo ya kupumua katika mtaa wa Uhuru, Nairobi.

Marehemu alitambuliwa kama Boniface Mutua Zangi, 53.

Chanzo kifo chake bado hakijajulikana.

Hatimaye, fundi mmoja wa vyuma mwenye umri wa miaka 23 alipatikana akiwa amefariki ndani ya karakana yake katika kile kinashukiwa kupigwa na umeme.

Polisi walisema mfanyikazi mwenza katika karakana hiyo ambaye alikuwa ametoka nje alirudi na kupata mwili wa Andrew Mutuora ukiwa ukiwa umelala sakafuni.

Alikimbia na kuzima umeme kwenye karakana na kumpeleka hospitali ambapo alitangazwa kuwa amefariki alipofika.

Polisi walitembelea eneo la tukio na mwili huo ulikuwa na michubuko kwenye mikono yote miwili, shingoni na kwenye viwiko ikiwa ni dalili za mapambano.

Mwili huo ulihamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri uchunguzi zaidi na uchunguzi wa maiti.