logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mahakama ya Rwanda yamzuia kiongozi wa upinzani kuwania urais

Bi Ingabire alifungwa kwa miaka minane na kusamehewa na Rais Kagame mwaka 2018.

image
na Davis Ojiambo

Habari14 March 2024 - 04:31

Muhtasari


  • • Kiongozi huyo wa upinzani Victoire Ingabire alikuwa mehukumiwa miaka 15 lakini alisamehewa na Kagame baada ya miaka minane gerezani.
  • • Bi Ingabire alitarajia kushindana na rais katika uchaguzi ujao.
Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda Victoire Ingabire.

Mahakama kuu katika mji mkuu wa Rwanda Kigali imetupilia mbali ombi la kiongozi maarufu Victoire Ingabire kutaka kurejeshewa haki zake zote za uraia ambazo zitamruhusu kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwezi Julai.

Bi Ingabire aliwaambia waandishi wa habari nje ya mahakama kwamba mahakama ya Rwanda "iko mbali na uhuru" ikiwa sheria ya juu (katiba) ilimpa haki, "lakini jaji leo aliegemeza uamuzi wake juu ya amri ya rais".

Bi Ingabire ambaye amefungwa kwa miaka minane na kusamehewa na Rais Paul Kagame mwaka 2018 kabla ya kukamilisha kifungo chake cha miaka 15, alitarajia kushindana na rais katika uchaguzi ujao.

"Sikubaliani na kile jaji alisema, na kwa bahati mbaya huwezi kukata rufaa kabla ya miaka miwili ... Bado tuko mbali na nchi inayotii sheria" aliwaambia waandishi wa habari.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved