logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Serikali yatafuta idhini ya kutumia bilioni 10 kukabiliana na mafuriko

Mvua hiyo isiyokoma imeharibu mazao na mali huku serikeli ikitenga makazi ya muda kwa watu waliohama makwao.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri06 May 2024 - 06:05

Muhtasari


•Bunge la taifa nchini Kenya kuidhinisha shilingi bilioni 10.6 kwa ajili ya kukabiliana na dharura ya mafuriko na misaada ya kibinadamu.

•Mvua hiyo isiyokoma imeharibu mazao na mali huku serikeli ikitenga makazi ya muda kwa watu waliohama makwao.

Bunge la taifa nchini Kenya kuidhinisha shilingi bilioni 10.6 kwa ajili ya kukabiliana na dharura ya mafuriko na misaada ya kibinadamu kwasababu ya mvua kubwa inayoendelea kunyesha kote nchini humo.

Maelezo ya fedha hizo yapo kwenye bajeti ya II ya ziada katika kipindi cha mwaka wa fedha mwaka 2023/2024.

Kufikia Jumamosi zaidi ya watu 228 walikuwa wamefariki dunia kutokana na mafuriko na maelfu ya watu kujeruhiwa huku wengine wengi wakilazima kuhama makazi yao.

Mvua hiyo isiyokoma imeharibu mazao na mali huku serikeli ikitenga makazi ya muda kwa watu waliohama makwao.

Hatua hii inafuatia tangazo ya mamlaka ya hali ya hewa la kunyesha kwa mvua kubwa katika maeneo mengi kote nchini humo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved