logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Gachagua azungumza kuhusu hali ya uhusiano wake na rais Ruto

Kulikuwa na dhana kuwa Gachagua na Ruto hawana uhusiano mzuri.

image
na SAMUEL MAINA

Habari27 May 2024 - 04:41

Muhtasari


  • •Akizungumza Jumapili wakati wa Ibada ya Kanisa huko Kesses, Gachagua alisema kuwa Rais amempa majukumu mengi ya kusimamia.
  • •Kulikuwa na dhana kuwa Gachagua na Ruto hawana uhusiano mzuri. 
akizungumza wakati wa ibada ya kanisa katika Shule ya Msingi ya Matharu iliyoko Kesses, Kaunti ya Uasin Gishu mnamo Mei 26, 2024.

Naibu Rais Rigathi Gachagua amethibitisha kuwa uhusiano wake na Rais William Ruto uko imara na wanashirikiana vilivyo.

Gachagua alisisitiza kuwa serikali ingali imara na inapiga hatua kubwa katika kutimiza ahadi zake kwa wakenya.

Akizungumza Jumapili wakati wa Ibada ya Kanisa huko Kesses, Gachagua alisema kuwa Rais amempa majukumu mengi ya kusimamia.

"Tupendane tuungane tuishi kwa amani, sisi sote ni wa Kenya na tukifanya namna hiyo tutaishi vizuri. Hio ndio Rais ametuongoza. Mimi na Rais tunafanya kazi nzuri, tunapendana kupanga kazi yetu. Amenipatia kazi nyingi hata ingine inanishinda, ameniwezesha kuendelea na kazi yangu kwa hivyo hivyo. serikali yetu iko imara tunaendelea na kazi," Gachagua alisema.

Kulikuwa na dhana kuwa Gachagua na Ruto hawana uhusiano mzuri. Pia alikuwa miongoni mwa viongozi waliomzidikisha Ruto akienda katika ziara yake ya Marekani.

Msemaji wa Ikulu Hussein Mohammed pia alipuuzilia mbali ripoti hizo akisema viongozi hao wawili hawana suala lolote.

Hussein alitupilia mbali hali hiyo alipokuwa akijibu maswali wakati wa mkutano na wanahabari kuhusu safari ya Ruto nchini Marekani.

"Kwa ufahamu wangu, hakuna shida kati ya Rais na Naibu wake," Hussein alisema.

“Ofisi ya Naibu Rais ni ofisi yenye uwezo na uwezo wote. Ukitaka kuuliza swali lolote au kujua chochote kuhusu Naibu Rais, unaweza kupata hapo.”

Mnamo Mei 21, Gachagua alifichua kwamba alikuwa amechukua siku saba kwenda katikati mwa msitu wa Mlima Kenya kwa maombi, kufunga na kutafakari.

"Nilikuwa nimechukua siku saba kwa maombi, kufunga, kutafakari, na hakuna simu na hakuna mtu angeweza kunisumbua. Ilinibidi kutafakari hali ya taifa na ustawi wa eneo hili,” Gachagua alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved