logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamume akamatwa kwa tuhuma za kuwalaghai wanaotafuta kazi, Migori

mshukiwa huyo alikuwa anajishirikisha katika tuhuma ya ulaghai kwa minajili ya kuwaibia wananchi

image
na Davis Ojiambo

Habari14 June 2024 - 08:21

Muhtasari


  • •Mshukiwa huyo alikuwa anajishirikisha katika tuhuma ya ulaghai kwa minajili ya kuwaibia wananchi wanaotauta kazi
  • •Afisa mkuu mtendaji wa bodi ya utumishi wa umma kaunti ya Migori amewatahadharisha wananchi kuwa makini wanapotafuta kazi
mkenya akamatwa kwa kumiliki kwa kuwalaghai wanachi

Polisi kwa ushirikiano na bodi ya utumishi wa umma katika kaunti ya Migori, wamemtia mbaroni mshukiwa mmoja wa mwenye umri wa makamu wa kiume kwa madai ya ulaghai na utapeli wa kujifanya mmojawapo wa wanachama wa bodi hiyo ya utumishi wa umma wa kaunti ya Migori.

Inasemekana kuwa, mshukiwa huyo alikuwa anajishirikisha katika tuhuma ya ulaghai kwa minajili ya kuwaibia wananchi waliokuwa kwenye pilkapilka za kutafuta kazi kwenye kaunti ya Migori.

Kulingana na Andrew Okatch, Afisa Mkuu Mtendaji wa bodi ya utumishi wa umma katika kaunti ya Migori, mshukiwa alikamatwa katika kituo cha uchukuzi na biashara cha Masara kwenye gatuzi ndogo ya Suna Magharibi.

Maafisa wa polisi wamekuwa kwenye pilkapilka za kumsaka kwa muda mpaka pale walipo mtia mbaroni.

Fauka ya hayo, Okatch aling’amua kuwa mshukiwa yumo korokoroni ambapo anangojewa kujibu mashtaka ya madai dhidi yake yanayomkabili.

Vilevile, Okatch alisema kuwa, mmojawapo ya waja waliotapeliwa alishaandikisha taarifa kwa kituo cha polisi.

Okatch pia, alisema kuwa aliandikisha taarifa ya ujumbe wa utapeli kwa kituo cha kurekebisha maadili kwa niaba ya bodi na wanachama wote waliohusishwa kwenye mzozo huo .

Afisa huyo mkuu mtendaji wa bodi ya utumishi wa umma kaunti ya Migori,vilevile, amewatahadharisha wananchi wa kaunti ya Migori wachukue tahadhari na umakini hasa wanapojishiriksha na shughuli za kutafuta kazi wasije wakajutia kwa kwikwi na simanzi wanaponaswa na mtego huu mzito wa utapeli.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved