logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamume apigwa na radi Kakamega akiwa kando ya jikoni

Wafanyibiashara wenza wa soko la Shianda walimkumbuka marehemu kama mwenye bidii na ukakamavu.

image
na Davis Ojiambo

Habari19 June 2024 - 07:19

Muhtasari


  • • Mkasa huo ulimfika masaa ya jioni mnamo 7.30 pm ya Jumanne. 
  • •Marehemu, Rashid Ondewa, alikuwa amesimama kando ya jikoni wakati radi ilimfika na kumfisha.
  • •Wafanyibiashara wenza walimkumbuka marehemu kama mfanyibiashara mwenye bidii na ukakamavu

Mtu mmoja katika kaunti ya Kakamega eneo bunge la Mumias Mashariki amefariki kufuatia kupigwa na radi masaa ya jioni.

Mwanamume huyo mwenye umri wa makamu inasemekana kwamba, alikuwa nyumbani kwake eneo la  Eshilarumwa wakati mkasa huo ulipomfika na kumfisha.

Ripoti zaidi, vilevile, zinaashiria kuwa mkasa huo ulimfika masaa ya jioni mnamo 7.30 pm ya Jumanne.

Marehemu, Rashid Ondewa, alikuwa amesimama kando ya jikoni wakati radi ilimfika na kumfisha kwa mujibu wa jamaa yake Tahiri Omumasaba.

Juhudi na jitihada za kumfikisha zahanatini ziliambulia patupu kwani Ondewa alifariki kwenye shughuli na pilkapilka za kumfikisha hospitalini na kuokolewa. Waama, mkono mtupu haurambwi.

“Ameondoka na kuacha pengo kubwa isillojazilika katika familia yetu. Rashid alikuwa nguzo adhimu katika familia yetu,” aliongeza Omumasaba huku akizungumza na Citizen.

Wafanyibiashara wenza wa soko la Shianda ambapo marehemu alikuwa akifanya kazi walimkumbuka marehemu kama mfanyibiashara mwenye bidii na ukakamavu wa kuigwa na kupigiwa mfano.

Mola ailaze roho yake mahali pema peponi na vilevile aifariji familia, jamaa na marafiki.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved