Illuminati wanafadhili maandamano ya Gen Z Nairobi – MP wa Gatundu South Gabriel Kagombe

"Wale watu wanasponsor maandamano hapa Nairobi ni ile group inaitwa illuminati na sijui mnajua illuminati ni kina nani. Na watoto wetu wamefungwa macho,”mbunge Kagombe alisistiza.

Muhtasari

• "Wale watu wanasponsor maandamano hapa Nairobi ni ile group inaitwa illuminati na sijui mnajua illuminati ni kina nani. Na watoto wetu wamefungwa macho,”mbunge Kagombe alisistiza.

•Mbunge Kururia Njoroge aliwasuta vijana kwa kusema," kama unaupinga mswada , achia madem wasupa, wanaume wenye wanalipa ushuru."

Mbung Gabriel Kagombe
Image: Hisani

Mbunge wa Gatundu Gabriel Kagombe, amejitokeza hadharani na kuwaambia wananchi kuwa maandamano ya vijana machachari wa Gen Z yanafadhiliwa na kundi  linalojulikana ‘Illuminati’.

Akizungumza Kagombe, alikuwa na haya ya kusema, “ kwa haya mambo ya finance bill, pasiwe mtu anachukua wakati huu kupotosha wananchi.

"Mkitaka kujua mtaona zile video zinazunguka hapa zinaanza na kitu inaitwa illuminati na ninajua hawa watu mumewaona. Wale watu wanasponsor maandamano hapa Nairobi ni ile group inaitwa illuminati na sijui mnajua illuminati ni kina nani. Na watoto wetu wamefungwa macho.”

Fauka ya hayo, mbunge Kururia Njoroge aliwasuta vijana kwa kusema," kama unaupinga mswada , achia madem wasupa, wanaume wenye wanalipa ushuru."

Ni suala linalozidi kuchipuka na kuleta mdahalo mkali kuhusu ni nani anayefadhili maandamano ya vijana machachari wa kizazi cha Gen Z.

Maandamano hayo yamezidi kuibua hisia mbalimbali huku wabunge kutoka mrengo wa Kenya Kwanza hasa wakisisitiza kuwa maandamano hayo yamefadhiliwa.

Hapo awali,  mbunge wa Dagoretti Kusini bwana Kiarie alisisitiza kuwa picha zilizokuwa zikisambazwa mtandaoni hazikuwa za waanadamanaji wa Kenya.

Vilevile kiongozi wa wengi katika bunge Kimani Ichungw'ah aliwashutumu hapo awali vijana hawa kwa kujishirikisha kwenye maandamano hayo kwani vijana wenye simu za IPhone na wanaopanda uber na kula KFC  ndio wanaojishirikisha kwenye maandamano hayo.

Maandamano haya yameibua hisia tofauti huku kundi la waandamanaji likishuhuduwa hii leo eneo la CBD wakiwa na vibango vya kukashifu maandamano yanayotarajiwa kuzuka mnamo Jumanne.

Kulingana na vijana, maandamano ya kuupinga mswada wa mwaka 2024 hayafadhiliwi na mtu yeyote wala viongozi wowote na kwamba wanatumia haki yao ya uhuru wa kuandamana kulingana na kipengee cha 37 cha katiba.