logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ng'ombe saba na kondoo tisa waaga kufuatia mkasa wa moto Siaya

wahalifu waliteketeza kwa moto zizi la ng'ombe la familia hiyo, na kusababisha wanyama kuteketea kupindukia.

image
na Davis Ojiambo

Habari24 June 2024 - 13:40

Muhtasari


  • •Wahalifu waliteketeza kwa moto zizi la ng'ombe la familia hiyo, na kusababisha wanyama kuteketea kupindukia.
  • • Aliongeza kwamba aliweza kumuokoa kondoo mmoja peke yake
  • •Familia wanashuku moto ulisababishwa na jirani yao ambaye amekuwa na matatizo na mhudumu 

Polisi katika eneo la Gem, Kaunti ya Siaya, wanachunguza tukio moja ambalo limewaacha wengi vinywa wazi ambapo familia moja iliwapoteza ng'ombe saba na kondoo tisa kufuatia  tukio la mkasa wa moto ambao ulitokea kwenye kitongoji cha Murumba mnamo usiku wa kuamkia leo.

Wakazi wanaamini kwamba wahalifu waliteketeza kwa moto zizi la ng'ombe la familia hiyo, na kusababisha wanyama kuteketea kupindukia.

Mhudumu wa nyumba aliiambia Citizen kwamba aliamshwa na mayowe ya majirani majira ya saa kumi asubuhi na kuarifiwa kuwa zizi la ng'ombe lilikuwa likiwaka moto.

Alipowasili kwenye mkasa huo, alikuta tayari limezidiwa na moto mkali na wanyama wote ndani yake.

Kupitia msaada wa wenyeji, mhudumu alijitahidi kwa udi na uvumba kuzima moto huo ila juhudi na jitihada zao ziliambulia patupu mighairi ya mafanikio.

Vilevile, aliongeza kwamba aliweza kumuokoa kondoo mmoja peke yake.

Familia inasema kuwa wanashuku moto ulisababishwa na jirani yao ambaye amekuwa na matatizo na mhudumu huyo na kwamba wanataka uchunguzi ufanyike na jirani huyo achunguzwe.

Naibu chifu wa eneo hilo, Millicent Otieno, alilaani tukio hilo na kusema kuwa uchunguzi tayari umeanzishwa kuhusu suala hilo.

Alionya kwamba washukiwa watapatikana na kufikishwa mbele ya sheria.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved