Wakenya kutoka maeneo ya Kisumu,Kisii, Mombasa na sehemu nyingine za nchi wamejitokeza barabarani ili kuonyesha kutoridhika kwao na serikali ya Rais Ruto.
Kauli mbiu ya #occupystatehouse imekuwa ikipamba moto kwenye mtandao wa kijamii wa X huku hali ya anga ikiwa haijulikani Nairobi.
Barabara zinazoelekea katika ikulu ya rais zimefungwa ili kuwazuia waandamanaji wanaokadiria kuzuru ikulu ya rais hii leo.
Fauka ya hayo ,maafisa wa Vikosi vya Ulinzi vya Kenya (KDF) wameonekana katika maeneo tofauti ya jiji kuu la Nairobi huku wakiwa na zana za vita licha ya mjadala mkali kuzuka kuhusu kuwekwa kwa maafisa wa KDF katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Hata hivyo, hali ya utulivu imeshuhudiwa katika maeneo mengine ya nchi ikiwemo Nairobi ambapo maandamano makali yalishuhudiwa mnamo Jumanne.
“Siku ya leo inakaa mbaya tuko kwa maandamano tuseme vijana wetu walikufa waliuwawa bila sababu hata sasa hatujapewa jibu tunalia bado sio eti hatulii hata kama tuko kazi.” Alisema mama mboga Linet Moraa akizungumza na Citizen.
Mswada wa kuidhinisha kuwekwa kwa majeshi ya KDF na bunge uliibua hisia chungu nzima huku mbunge wa Rarieda Otiende Amollo akikosoa uamuzi huo akisema kuwa ni kinyume na katiba ya kenya.
Vilevile, alisema kuwa wabunge walioidhinisha mswada huo haikufika 50 namna katiba inavyoagiza na pia ukosefu wa utangazaji kama ilivyo kawaida katika upeperushaji wa miswada ya kitaifa kama ilivyo kawaida.
“Ruto aache kuwadanganya wakenya . Rais aache kudanganya wakenya. Tumesoma bwana! Katika katiba ya Kenya rais ana majukumu mawili ya kukataa ama kukubali hakuna kitu kama kutoa mswada,” alisema mwandamanaji mmoja katika kaunti ya Mombasa akiiambia NTV.
Mbali na hayo, wananchi wametulia huku wakingoja kung’amua hali itakavyokua nchini