logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Msiba huku OCPD wa Kuria Mashariki akijitoa uhai kwa kujipiga risasi kimakosa

Lakini jinsi tahadhari zinavyofanywa zinaweza kugeuka kuwa mbaya, wakati mwingine, maafisa walisema.

image
na SAMUEL MAINA

Habari02 July 2024 - 08:39

Muhtasari


  • •Polisi alifariki baada ya bastola aliyokuwa akiishika kudaiwa kutoa risasi iliyomuua katika kituo cha polisi cha Kegonga, Kuria, Kaunti ya Migori.
  • •Lakini jinsi tahadhari zinavyofanywa zinaweza kugeuka kuwa mbaya, wakati mwingine, maafisa walisema.
Bunduki

Polisi wanachunguza hali ambayo afisa mkuu wa polisi alifariki baada ya bastola aliyokuwa akiishika kudaiwa kutoa risasi iliyomuua katika kituo cha polisi cha Kegonga, Kuria, Kaunti ya Migori.

Superintendent James Mugo Kabachia ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Kuria Mashariki alipoteza damu kufuatia jeraha alilopata Julai 1 jioni.

Tukio hilo lilitokea saa kumi jioni ya Jumatatu alipokuwa akipokea silaha hiyo kwa shughuli za usiku.

Polisi walisema alikuwa akipokea bastola kutoka kwa ghala la silaha la kituo na alikuwa akichukua tahadhari za usalama kwenye silaha hiyo ilipofyatua risasi na kumjeruhi vibaya.

Afisa ambaye alisimamia ghala hilo la silaha aliripoti kuwa alimpa Mugo bastola aina ya Berreta iliyokuwa na risasi 15 alipoamua kufanya ukaguzi wa usalama kwenye silaha hiyo.

Ukaguzi wa tahadhari ni wa kawaida na ni muhimu kwa wamiliki kuwa na uhakika wa usalama wa silaha.

Lakini jinsi tahadhari zinavyofanywa zinaweza kugeuka kuwa mbaya, wakati mwingine, maafisa walisema.

Hapo ndipo aliporipotiwa kutoa risasi moja kutoka kwenye silaha iliyojigonga kwenye sehemu ya paja la kulia.

Risasi ilitoka kwenye kitako cha kulia na kukamata mshipa muhimu, maafisa walisema.

Mugo alikimbizwa katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Kegonga na baadaye akapewa rufaa katika Hospitali ya Kaunti ya Migori ambapo alitangazwa kuwa amefariki alipofika.

Wenzake walisema alivuja damu nyingi jambo ambalo linaaminika kusababisha kifo hicho.

Mwili wa marehemu ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.

Polisi walisema wanakusudia kuchunguza jinsi tukio hilo lilivyotokea.

Mashahidi na watoa majibu wa kwanza ni miongoni mwa watakaohojiwa kuhusu tukio hilo.

Timu kutoka Migori ilitumwa kuungana na wale waliokuwa mashinani kuchunguza tukio hilo, maafisa walisema.

Ajali kama hizo ni za kawaida ndani ya huduma. Viongozi wanaziita ajali.

Familia ya afisa huyo iliarifiwa kuhusu mkasa huo.

Utafsiri: Samuel Maina


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved