logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ruto atoa wito wa kuangaliwa upya kwa nyongeza ya mishahara ya maafisa wa serikali

Hatua hii ni baada ya notisi ya gazeti la serikali ya Agosti 9, 2023, ya SRC kutangaza nyongeza ya mishahara.

image
na Davis Ojiambo

Habari04 July 2024 - 05:07

Muhtasari


  • • Mabadiliko hayo yamezua taharuki kwa umma huku kukiwa na kilio cha kupunguza matumizi ya umma.

Rais wa Kenya William Ruto ametaka kuangaliwa upya mara moja kwa mapendekezo ya nyongeza ya mishahara kwa maafisa wa serikali akitaja haja ya hatua za kubana matumizi.

Hatua hii ni baada ya notisi ya gazeti la serikali ya Agosti 9, 2023, ya Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC) kutangaza mapitio ya nyongeza ya mishahara ya Watendaji na Wabunge kuanzia Julai 1, 2024.

Mabadiliko hayo yamezua taharuki kwa umma huku kukiwa na kilio cha kupunguza matumizi ya umma.

Ruto, kupitia kwa msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed, aliagiza Hazina ya Kitaifa kukagua notisi ya gazeti la serikali kwa kuzingatia Muswada wa Fedha wa 2024 ulioondolewa sasa na vikwazo vya kifedha vinavyotarajiwa katika mwaka wa kifedha wa 2024/25.

"Rais amesisitiza kuwa huu ni wakati, zaidi ya hapo awali, kwa Watendaji na vyombo vyote vya serikali kuishi kulingana na uwezo wao," alisema Mohamed kwenye X.

Waziri wa Utumishi wa Umma Moses Kuria pia ameeleza kuwa licha ya SRC kupewa jukumu la kukagua mishahara mara kwa mara kwa maafisa wote wa serikali, inapaswa kudumisha hatua za kubana matumizi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved