Washukiwa wanne wakamatwa na bidhaa zilizoibiwa katika duka la mbunge wa Kieni

"Hii ni baada ya taswira yake kunaswa katika rekodi za simu zilizosambazwa akiiba kwenye duka kuu," alisema DCI.

Muhtasari
  • Moses Gachwe, 30, alipatikana katika nyumba nyingine na suruali 22 za kaki, fulana 9, nguo za ndani 24 (mabondia) na viatu vilipatikana kwenye eneo hilo.
Washukiwa wanne wakamatwa na bidhaa zilizoibiwa katika duka la mbunge wa Kieni
Image: DCI/ X

Washukiwa zaidi wamenaswa katika msako unaoendelea wa kuwasaka wahuni waliopora na kuchoma maduka makubwa ya Chieni kaunti ya Nyeri na Nanyuki wakati wa maandamano ya kitaifa mnamo Juni 25.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai (DCI) alisema Alhamisi kwamba washukiwa hao wanne walifukuzwa kutoka maficho tofauti huko Nanyuki na walipatikana wakiwa na baadhi ya bidhaa zilizoibwa.

Chris Wamuhu, 24, alikamatwa katika nyumba ya kukodisha na alipatikana akiwa na friji ya Hisense iliyoibiwa, mashine ya kutolea maji ya Uken, vikombe vya kahawa, vijiko, vyombo vya moto, sahani za luminarc miongoni mwa vingine.

"Hii ni baada ya taswira yake kunaswa katika rekodi za simu zilizosambazwa akiiba kwenye duka kuu," alisema DCI.

Moses Gachwe, 30, alipatikana katika nyumba nyingine na suruali 22 za kaki, fulana 9, nguo za ndani 24 (mabondia) na viatu vilipatikana kwenye eneo hilo.

"Katika viunga vya mji wa Asian Quarters, Charles Kaariri Mumbi mwenye umri wa miaka 35 pia alikamatwa akiwa na baiskeli ndogo, wakati John Ndirangu Ndirirtu, 41, alipatikana na flasks sita , toroli ya ununuzi, friji ya LG na sahani kadhaa za luminarc na vikombe," DCI alisema.

Wanne hao wataungana na washukiwa wengine ambao tayari wako chini ya ulinzi wa polisi huku maafisa wakiapa kuwakabili washukiwa hao zaidi.