Charlene Ruto ampongeza babake, Rais Ruto kwa kuzungumza na vijana kwenye X space

“Najivunia Rais wetu kwa kuchukua muda wa kusikiliza na kujibu kero za vijana kwenye X space jana!" Charlene alisema.

Muhtasari

•Binti huyo wa rais mwenye umri wa miaka 31 alibainisha kuwa anajivunia baba yake kuzungumza na vijana kwenye jukwaa la X space.

•Pia aliwataka wale waliojiunga na kipindi cha rais kutoa maoni yao ya ukweli na fikiria zao juu yake.

Charlene Ruto
Binti ya rais William Ruto, Charlene Ruto
Image: HISANI

Charlene Ruto, binti  wa rais wa Kenya, William Samoei Ruto ameelezea hisia zake kuhusu baba yake kuwashirikisha vijana katika mazungumzo kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Katika taarifa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, binti huyo wa rais mwenye umri wa miaka 31 alibainisha kuwa anajivunia baba yake kuzungumza na vijana kwenye jukwaa la X space.

Pia aliwapongeza vijana waliozungumza na rais akiatambua kwamba walifanya hivyo kwa ukweli na heshima.

“Najivunia Rais wetu kwa kuchukua muda wa kusikiliza na kujibu kero za vijana kwenye X space jana! Pia ninajivunia sana vijana kwa kujieleza ukweli na heshima. Tulifanya hivyo!,” Charlene alisema Jumamosi.

Pia aliwataka wale waliojiunga na kipindi cha rais kutoa maoni yao ya ukweli na fikiria zao juu yake.

Siku ya Ijumaa alasiri, Rais Ruto alizungumza na vijana katika kipindi cha X Space ambapo aliibua maswali mazito kutoka kwa wazungumzaji.

Ruto alisema alikubali kuondoa Mswada wa Fedha wa 2024 kwa sababu Wakenya walisema hawakuutaka.

Rais aliongeza kuwa Mswada wa Fedha ulijaa "uongo na propaganda", na akakana, kwa mfano, kuwa kulikuwa na sehemu kuhusu kuongeza viwango vya ardhi na kodi

“Niwaambie, hakuna sentensi hata moja katika Muswada wa Sheria ya Fedha inayozungumzia kodi ya ardhi na masuala ya ardhi,” alisema.

Ruto pia alikanusha kuwa kulikuwa na mapendekezo ya ushuru katika Mswada wa wagonjwa wa saratani.

“Niwaambie kwamba kwa kweli katika Muswada huu wa Sheria ya Fedha, tulikuwa tumeweka Sh2 milioni kuwalipa watu walio na saratani, kisukari na shinikizo la damu chini ya Mpango wetu wa Afya kwa Wote,” Rais alisema.

Kundi la Gen Z liliunda idadi kubwa ya waandamanaji waliovamia barabarani kupinga Mswada wa Fedha uliopingwa.

Rais alikubali shinikizo na kukataa kutia saini Muswada huo kuwa Sheria na kulitaka Bunge kufuta vifungu vyote.