logo

NOW ON AIR

Listen in Live

David Chege, mmoja wa vijana waliouawa wakati wa maandamano azikwa

Chege alikuwa miongoni mwa wakenya waliouawa kwa kupigwa risasi nje ya majengo ya bunge.

image
na Davis Ojiambo

Habari10 July 2024 - 05:06

Muhtasari


  • • Mwanaharakati Boniface Mwangi aliwasihi Wakenya kuendeleza vita dhidi ya uongozi mbaya.
  • • Serikali inashikilia kuwa ni  watu 25 pekee waliuawa katika maandamano kote nchini, na kupinga takwimu za Mashirika ya Haki za binadamu.
  • • Mashirika ya Haki za binadamu yalisema kuwa zaidi ya watu 40 walifariki.

David Chege, mmoja wa vijana waliouawa wakati wa maandamano ya kupinga msuada wa fedha nchini, alizikwa siku ya Jumanne nyumbani kwao eneo la Gatundu.

Chege ambaye alipigwa risasi kichwani alikuwa mtaalamu wa IT na mwalimu wa Sunday School katika Kanisa la Jubilee Christian Church.

Chege alikuwa miongoni mwa wakenya waliouawa kwa kupigwa risasi nje ya majengo ya bunge wakati waandamanaji walipozidi polisi nguvu na kuingia katika majengo ya bunge.

Mazishi yake yalihudhuriwa na wanaharakati wengi miongoni mwao  Boniface Mwangi, Hanifa Adan  na Khalid Hussein wa Haki Afrika.

Wakati wa mazishi wanaharakati waliikabidhi familia yake bendera, wakisema kuwa marehemu Chege alilipa gharama kubwa kwa uzalendo wake.

Mwanaharakati Boniface Mwangi aliwasihi Wakenya kuendeleza vita dhidi ya uongozi mbaya, akiwataka wabadilishe picha ya Rais Ruto na picha ya bendera ya Kenya.

Serikali inashikilia kuwa ni  watu 25 pekee waliuawa katika maandamano kote nchini, na kupinga takwimu za Mashirika ya Haki za binadamu ambayo yalisema kuwa zaidi ya watu 40 walifariki.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved