Rais Ruto kuhutubia taifa kwa mara nyingine leo saa nane alasiri

Agenda ya kikao cha rais na waandishi wa habari, hata hivyo, bado haijulikani.

Muhtasari

•Kulingana na Katibu wa Habari wa Ikulu Emmanuel Talam, Rais atahutubia nchi kutoka Ikulu ya Nairobi.

Rais William Ruto
Image: MAKTABA

Rais William Ruto anatarajiwa kuhutubia taifa saa nane mchana.

Kulingana na Katibu wa Habari wa Ikulu Emmanuel Talam, Rais atahutubia nchi kutoka Ikulu ya Nairobi.

Agenda ya kikao cha rais na waandishi wa habari, hata hivyo, bado haijulikani.

Ruto mnamo Ijumaa alidokeza kutekelezwa kwa baadhi ya mabadiliko katika serikali hivi karibuni.

Alitoa dokezo hilo wakati wa hotuba kwa taifa ambapo alitangaza hatua kadhaa za kubana matumizi ili kuokoa gharama serikalini.

Hotuba ya Alhamisi inajiri siku tatu tu baada ya Ruto na kiongozi wa Upinzani Raila Odinga kuitisha mazungumzo ya kitaifa kuanzia Jumatatu, Julai 15.

Mazungumzo hayo yatakuwa na angalau washiriki 150, kati yao 50 wakiwakilisha vijana.

Baada ya wito huo, baadhi ya wanasiasa wa Upinzani walisema hawatakuwa sehemu ya kikao hicho.