logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rais Ruto ameahidi fedha zaidi kwa idara ya polisi

Alisema serikali yake itatoa msaada unaohitajika kwa polisi ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa umma.

image
na SAMUEL MAINA

Habari26 July 2024 - 09:16

Muhtasari


  • •Alisema serikali yake itatoa msaada unaohitajika kwa polisi ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa umma.
  • •“Serikali inajitolea kusaidia idara ya polisi katika kuipatia vifaa na teknolojia ya kisasa ili kuongeza ufanisi wake katika kutekeleza majukumu yake,” alisema Rais William Ruto.

Rais William Ruto, mnamo Ijumaa, ametangaza kwamba utawala wake utaongeza fedha zaidi kwa jeshi la polisi ili kusaidia katika kutatua baadhi ya changamoto za kimfumo zinazoweza kuwa zinawakabili maafisa hao.

Akizungumza wakati wa mkutano na mainspekta jenerali wapya wa polisi, Rais alisema kwamba uwekezaji wa ziada katika Huduma ya Polisi ya Kitaifa utaimarisha utendaji wa polisi katika shughuli zao za kila siku.

Alisema serikali yake itatoa msaada unaohitajika kwa polisi ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa umma.

“Serikali inajitolea kusaidia idara ya polisi katika kuipatia vifaa na teknolojia ya kisasa ili kuongeza ufanisi wake katika kutekeleza majukumu yake,” alisema Rais William Ruto.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa ingawa rasilimali zaidi zitapelekwa katika shughuli za polisi, wanapaswa kufanya kazi zao ndani ya mipaka ya sheria vilevile kwa mujibu wao kulingana na katiba ya Kenya.

“Tunaomba polisi wafanye shughuli zao kwa weledi na uaminifu,” alisema Rais Ruto.

Rais alitamba haya alipokuwa akiapisha manaibu wa mainspekta jenerali kina Eliud Lagat atakayeshikilia Huduma ya Polisi ya Kenya ambapo naye Gilbert Masengeli atashika hatamu katika Huduma ya Polisi ya Utawala katika sherehe iliyoandaliwa kwenye Ikulu ya Rais iliyoko Kaunti ya Mombasa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved