Waumini wa Ahmadiyya woamba amani Kenya

Mwaka huu, kongamano la siku tatu linafanyika chini ya kaulimbiu ya ‘amani’.

Muhtasari

•Walifanya maombi maalum kwa ajili ya nchi wakati wa kongamano la hamsini na nane.

•Mkutano wa mwaka huu umevutia takriban waumini zaidi ya 40,000 wa Ahmadiyya kutoka maeneo na pande zote za dunia.

Kundi la waumini wa Ahmadiyya wa Kenya nchini Uingereza
Image: MAKTABA

Wakenya wamehimizwa kuunga mkonowito wa amani wakati nchi inakabiliana na maandamano makali dhidi ya serikali ya Rais Wiliam Ruto.

Waislamu wa Ahmadiyya kutoka Kenya walioshiriki katika mkutano wa kila mwaka wa Jalsa Salana nchini Uingereza walifanya maombi maalum kwa ajili ya nchi wakati wa kongamano la hamsini na nane.

Mkutano wa Jalsa Salana wa Ahmadiyya wa mwaka huu ulianza katika Alton Hampshire, Uingereza, ambapo maombi ya amani yalikuwa yakiendelea kutawala na kukithiri katika eneo hilo la Uingereza.

Mkutano wa mwaka huu umevutia takriban waumini zaidi ya 40,000 wa Ahmadiyya kutoka maeneo na pande zote za dunia.

Waumini wa Ahmadiyya wa Kenya walifanya maombi maalum kwa ajili ya nchi yao inayozidi kushuhudia mapinduzi hasa kutoka kwa vijana.

Wakenya wamehimizwa kufikiria suluhisho la amani kwa hali ya kisiasa ya sasa katika kutatua matakwa na madai yao.

Mwaka huu, kongamano la siku tatu linafanyika chini ya kaulimbiu ya ‘amani’.

Kiongozi wa kiroho wa Ahmadiyya, Hadhrat Mizra Masroor, ameitaka dunia kuwa na uvumilivu wa kisiasa na kidini kwa pamoja.

Waumini wa Ahmadiyya wanakabiliwa na mateso na kukataliwa ulimwenguni kote kutokana na imani zao na katika baadhi ya nchi wamezuiwa kujishirikisha na imani yao vilevile kuitwa Waislamu.