logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kenya yawasilisha rasmi hati za Raila za kugombea Uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika

Serikali ya Kenya imewasilisha rasmi nyaraka za kumuunga mkono mgombea wake, Raila Odinga

image
na Davis Ojiambo

Habari30 July 2024 - 05:15

Muhtasari


  • Vipaumbele vya Raila katika usukani wa AU vitajumuisha:
  • • Ushirikiano wa Afrika na Maendeleo ya Miundombinu,
  • • Mabadiliko ya Kiuchumi,
  • • Kuimarisha Biashara ya Ndani ya Afrika  na 
  • • Uhuru wa Kifedha.

Serikali ya Kenya imewasilisha rasmi nyaraka za kumuunga mkono mgombea wake, Raila Odinga, katika azma yake ya kuwa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC).

Wakiongozwa na Katibu Mkuu wa wizara ya mashauri ya kigeni Korir Sing'oei, wajumbe wa Kenya waliwasilisha hati hizo kwa Mkuu wa Kanda ya Mashariki, Dharmraj Busgeeth na kwa Ofisi ya Wakili wa Kisheria wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa.

Kulingana na Sing'oei, vipaumbele vya Raila katika usukani wa AU vitajumuisha; Ushirikiano wa Afrika na Maendeleo ya Miundombinu, Mabadiliko ya Kiuchumi, Kuimarisha Biashara ya Ndani ya Afrika, Uhuru wa Kifedha, Usawa wa Jinsia na Usawa, Mageuzi katika kilimo Hatua za Hali ya Hewa, Amani na Usalama na Ajenda ya kuwazesha vijana Afrika.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved