logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mazishi ya kiongozi wa Hamas yavutia umati mkubwa wa watu Iran

Maelfu walijitokeza kwa mazishi ya Ismail Haniyeh, ambaye aliuawa katika shambulizi mjini Tehran.

image
na Davis Ojiambo

Habari01 August 2024 - 12:11

Muhtasari


  • • Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Aliongoza sala kabla ya kiongozi huyo kuzikwa nchini Qatar.
  • Vyombo vya habari vya Marekani vimewanukuu maafisa wa Iran wakisema kiongozi huyo mkuu ameamuru shambulio la moja kwa moja dhidi ya Israel.

Maelfu wamejitokeza kuhudhuria mazishi ya kiongozi wa kisiasa wa Hamas, Ismail Haniyeh, nchini Iran ambaye aliuawa katika shambulizi mjini Tehran siku ya Jumatano.

Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, aliongoza sala kabla ya kiongozi huyo kuzikwa nchini Qatar.

Vyombo vya habari vya Marekani vimewanukuu maafisa wa Iran wakisema kiongozi huyo mkuu ameamuru shambulio la moja kwa moja dhidi ya Israel, na ndio chanzo cha shambulio lililotokea nchini Iran.

Israel haijatoa maoni yoyote kuhusu mauaji hayo moja kwa moja.

Hata hivyo, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema nchi yake imetekeleza "pigo kali" kwa maadui zake katika siku za hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na kuuawa kwa kamanda mkuu wa Hezbollah nchini Lebanon saa chache kabla ya shambulio la Tehran.

Alionya Waisrael kwamba "bado kuna changamoto siku za usoni", huku hofu ya mzozo mkubwa katika Mashariki ya Kati ikiongezeka.

"Tangu kutokea kwa shambulizi Beirut, tumesikia vitisho kutoka pande zote," alisema kwenye ujumbe uliopeperushwa kwenye Televisheni.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alionya dhidi ya "kuongezeka kwa hatari" kwa uhasama katika eneo hilo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved