Mpox sio kama covid inaweza kudhibitiwa - Mtaalamu

Hatua madhubuti lazima ichukuliwe sasa hivi - ikiwa ni pamoja na kuhakikisha chanjo zinafika maeneo yenye uhitaji mkubwa.

Muhtasari

• Virusi hivyo vinavyosababisha homa na upele vinaweza kusambazwa kwa kugusana na ngozi na vidonda, ikiwa ni pamoja na wakati wa kujamiiana.

Homa ya nyani yaani Mpox "sio Covid mpya", kwa sababu mamlaka zinajua wazi jinsi ya kudhibiti kuenea kwake, mtaalam mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni amesema.

Licha ya wasiwasi kuhusu aina mpya ya virusi, na tahadhari ya kimataifa, mkurugenzi wa kanda ya Ulaya Dk Hans Kluge amewaambia waandishi wa habari, pamoja tunaweza – na ni lazima - kukabiliana na mpox.

Na hatua madhubuti lazima ichukuliwe sasa hivi - ikiwa ni pamoja na kuhakikisha chanjo zinafika maeneo yenye uhitaji mkubwa – hiyo inaweza kukomesha mzunguko mwingine wa hofu.

Virusi vipya vya maambukizi haya, Clade Ib, vimethibitishwa nchini Uswidi wiki iliyopita na kuhusishwa na mlipuko unaoongezeka barani Afrika.

Mpox imeua takriban watu 450 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, iliyojulikana zamani kama Zaire, katika miezi ya hivi karibuni, ikiwa ni yenye kuhusishwa na virusi Clade Ib.

Bado kuna mengi ya kujifunza kuhusu kirusi kipya, wataalam wanasema, lakini vinaweza kuenea kwa urahisi na kusababisha ugonjwa mbaya zaidi.

Virusi hivyo vinavyosababisha homa na upele vinaweza kusambazwa kwa kugusana na ngozi na vidonda, ikiwa ni pamoja na wakati wa kujamiiana.