Shirika la uchapishaji vitabu KLB lapata mkurugenzi mpya

Aritho anachukua nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa sasa, Bw. Victor Lomaria ambaye muda wake unakamilika.

Muhtasari

• Aritho ataongoza shughuli za Ofisi hadi Mkurugenzi Mkuu Mkuu atakapoteuliwa.

Bw. Julius K. Aritho aliyeteuliwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Kenya Literature Bureau (KLB).
Bw. Julius K. Aritho aliyeteuliwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Kenya Literature Bureau (KLB).
Image: HISANI

Waziri wa elimu Julius Ogamba Migosi, amemteua Bw. Julius K. Aritho kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Kenya Literature Bureau (KLB) kwa muda wa miezi sita (6) kuanzia tarehe 1 Septemba 2024 hadi uteuzi wa Mkurugenzi mkuu wa kudumu.

 Aritho alikuwa amehudumu kama meneja wa ukaguzi wa mahesabu na meneja wa kifedha  katika shirika hilo.

Kulingana na taarifa iliyotiwa saini na mwenyekiti wa bodi ya usimamizi ya shirika la KLB Dkt. Rispah Wepukhulu, Aritho anachukua nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa sasa, Bw. Victor Lomaria ambaye muda wake wa utumishi unakamilika tarehe 31 Agosti 2024. Aritho ataongoza shughuli za Ofisi hadi Mkurugenzi Mkuu Mkuu atakapoteuliwa.

“Kufuatia tangazo hili, Bodi ya Usimamizi, ilifanya mkutano maalum tarehe 29 Agosti 2024 katika Ukumbi wa Bodi ya KLB huko South C, ili kuwasilisha uamuzi wa waziri kwa usimamizi mkuu Kuu wakati wa hafla ya kukabidhi”, taarifa hiyo ilisema.

“Nachukua fursa hii kumshukuru Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake, kwa matendo yake ya kujitolea ya utumishi ambayo yamefanya shirika hilo kuafikia ustawi wa sasa. Ninashukuru kujitolea kwa Bw. Lomaria kuimarisha ustawi wa wafanyakazi na kufanya KLB kituo kikuu cha uchapishaji,” taarifa hiyo ilieleza.

Wafanyikazi waliombwa kushirikiana na Aritho ili kurahisisha mpito wa usimamizi huku shughuli zikiendelea kwauteuzi wa mkurugenzi mkuu wa kudumu.