NPSC yasitisha hatua ya Msengeli kuwapindisha vyeo maafisa wa polisi

Mwenyekiti Eliud Kinuthia alimwagiza kaimu IG kusimamisha kwa muda upandishaji vyeo hadi kuteuliwa kwa Inspekta Jenerali mkuu.

Muhtasari

• Uamuzi huo unaonekana kuwa sehemu ya hatua zilizochukuliwa kushughulikia wasiwasi miongoni mwa baadhi ya maafisa.

Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Huduma ya Polisi Eluid Kinuthia na makamishna wengine wakati wa mkutano na wanahabari kuhusu sasisho kuhusu mishahara ya polisi na kupandishwa vyeo katika Jumba la CBK Pension Towers, Nairobi mnamo Septemba 5, 2024. Picha: LEAH MUKANGAI
Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Huduma ya Polisi Eluid Kinuthia na makamishna wengine wakati wa mkutano na wanahabari kuhusu sasisho kuhusu mishahara ya polisi na kupandishwa vyeo katika Jumba la CBK Pension Towers, Nairobi mnamo Septemba 5, 2024. Picha: LEAH MUKANGAI

Tume ya Kitaifa ya Huduma za Polisi (NPSC) imefutilia mbali upandishaji vyeo wote ulioidhinishwa hivi majuzi na kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli.

 Akihutubia wanahabari siku ya Alhamisi, mwenyekiti wa tume hiyo Eliud Kinuthia alimwagiza kaimu IG kusimamisha kwa muda upandishaji vyeo hadi kuteuliwa kwa Inspekta Jenerali mkuu.

 Uamuzi huo unaonekana kuwa sehemu ya hatua zilizochukuliwa kushughulikia wasiwasi miongoni mwa baadhi ya maafisa.

 "Hii itawezesha kutulia kwa wale waliopandishwa vyeo na uimarishaji wa amri katika miundo na vitengo mbalimbali vya huduma ya polisi" alisema. 

Jumla ya askari polisi 1,957 (wanaume 1, 870 na wanawake 87) wenye umri wa kati ya miaka 53-59 bila makosa ya kinidhamu wameidhinishwa na tume kwa ajili ya kupandishwa vyeo kwa kustahili vyeo mbalimbali. 

Tume hiyo iliidhinisha upandishaji vyeo kufuatia malalamiko ya kukwama kwa maafisa katika cheo kimoja.Hii ilikuwa hatua ya kuwapa motisha wanapokaribia umri wao wa kustaafu.