logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Waziri Opiyo Wandayi aelezea kwa nini umeme hupotea wakati wa mvua

Waziri wa kawi Opiyo Wandayi ameelezea sababu ambazo hufanya taifa kushuhudia ukosefu wa nguvu za umeme wakati wa mvua.

image
na Evans Omoto

Yanayojiri04 February 2025 - 14:55

Muhtasari


  • 'Kuna sababu kadhaa zinazosababisha kupotea kwa umeme kama kuzeeka kwa nyaya za umeme,vigingi ambapo haviwezi kustahimili mawimbi na mabadiliko ya anga 

Waziri wa kawi Opiyo Wandayi ameelezea sababu ambazo hufanya taifa kushuhudia ukosefu wa nguvu za umeme wakati wa mvua.

Akizungumza katika kituo kimoja cha runinga hapa nchini Wandai amesema kuwa hii hutokana na Vigingi na nyaya ambazo zimezeeka ndizo husababisha nguvu za umeme kupotea,Kulingana na mbunge huyo wa zamani wa Ugunja amesema mifumo ya miundombinu imekuwa hafifu kiwango kwamba haiwezi kustahimili hali ya anga.

'Kuna sababu kadhaa zinazosababisha kupotea kwa umeme kama kuzeeka kwa nyaya za umeme,vigingi ambapo haviwezi kustahimili mawimbi na mabadiliko ya anga vilevile waziri aliendelea kufafanua kuwa kama taifa wameekeza pakubwa kuhakikisha kuwa wanabadilisha hali nzima na kuwa na miundombinu ambayo ni dhabiti aliwarai wakenya kuwa na subira serikali inapoharakisha mpango wa kufanyia marekebisho mpango mzima.

''Hii ndio maana tumeanza kuekeza katika mifumo mipya ili tukabiliane na hali hii ambayo imekuwa ikiwahangaisha wakenya kwa hivyo tunawarai wakenya wawe na subira na watupe muda ili tushughulikie swala hili Wandayi alidokeza.''mnamo Jumamosi ya Agosti tarehe 3,2024 alipojiwasilisha mbele ya kamati ya kawi katika bunge la taifa Wandayi alidokeza kuwa iwapo angechukua hatamu ya uongozi angeangazia sana upande wa Magharibu ambao umeathirika sana na hii hali ya ukosefu wa umeme mara kwa mara .

Aliyekuwa kiongozi wa walio wachache bungeni alisema kuwa angehakikisha kuwa anaziangazia sehemu zile ambazo hazina umeme kabisa ili zishughulikiwe kwa dharura''nitapiga msasa mwanzo sehemu ambazo zinahitaji kuunganishiwa nguvu za umeme kisha nihakikishe watumizi wanapata kwa wepesi na kwa haraka''.

Waziri alikuwa akizungumza akirejelea kauli zake za kitambo kuwa wakati ule iwapo angechaguliwa angehakikisha kuwa mtambo wa nguvu za umeme wa Turkwel -Ortum Kitale unamalizika na kuwekwa katika matumizi mwafaka Waziri alikuwa anajibu swali aliloulizwa na mbunge wa Pokot Magharibi bwana David Pkosing.

Waziri anapoelezea hali ya umeme nchini itakubukwa vizuri kuwa idara yake pia imekuwa ikijitahidi kuhakikisha kuwa inashughulikia pia viwango vya gharama ya mafuta nchini ambapo kwa zaidi ya miezi miwili iliyopita bei ya mafuta ya petroli,diseli na mafuta taa imekuwa ikipungua kwa bei hatua baada ya hatua hivyo basi kawi ya umeme ni sharti ishughulikiwe vyema pia kwa sababu yuko ofisini na wakenya wanahitaji huduma bora kutoka kwa ofisi yake.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved