
Mtayarishaji maudhui ya YouTube mashuhuri , Nick Yardy, amezua mjadala mkali baada ya kudai kuwa anachumbiana na binti pamoja na mama yake.
Katika video iliyosambaa mitandaoni kwa kasi, Yardy alidai kuwa alikuwa amewapachika mimba wote wawili, , jambo lililoibua mshangao na ukosoaji mkubwa.
Hata hivyo, baada ya gumzo hilo kuzidi kupamba moto, mtayarishaji maudhui huyo alirejea na kufafanua kuwa madai hayo yalikuwa sehemu ya kipindi cha burudani, ingawa alisisitiza kuwa uhusiano wake wa kimapenzi na wanawake hao wawili ni wa kweli.
Katika video yake, alionekana akiwa na mpenzi wake Jade na mama yake Dani, akitangaza kuwa anatarajia watoto kutoka kwa wote wawili.
Tangazo hilo liliibua hisia kali, huku baadhi ya watu wakieleza mshtuko wao na wengine wakimshutumu kwa kuvuka mipaka ya maadili.
“Huu ni upuuzi wa hali ya juu! Kwanini watu wanafanya kila kitu kwa ajili ya 'views'?” aliandika mtumiaji mmoja wa X (zamani Twitter).
Mwingine aliongeza: “Hii ni aibu kubwa. Siku hizi mitandao imejaa watu wanaofanya chochote ili wapate umaarufu.”
Baada ya shinikizo kubwa, Yardy alijitokeza kufafanua kuwa madai ya ujauzito yalikuwa ya kubuni tu, lakini akasisitiza kuwa mahusiano yao ni ya kweli.
"Najua wengi hawataelewa, lakini hii ni sehemu ya
maudhui yangu ya burudani," alisema Yardy.
Aliongeza, "Nampenda Jade na Dani, na mahusiano yetu ni halali kabisa."
Yardy aliongeza kuwa hakutarajia watu kulichukulia jambo hilo kwa uzito:
"Tulitaka tu kuwapa mashabiki kitu cha kufurahia,
lakini haimaanishi kuwa uhusiano wetu si wa kweli," alisema.
Hii si mara ya kwanza kwa wanamitandao kuzua mijadala kwa madai tata ili kuvutia watazamaji.
Yardy, mwenye zaidi ya wafuasi milioni 2.9 kwenye YouTube, pamoja na maelfu wengine kwenye mitandao kama Instagram na TikTok, ameendelea kupata ufuasi mkubwa licha ya ukosoaji.
Wataalamu wa mitandao wanatahadharisha kuwa mienendo kama hii inaweza kupotosha vijana wanaomfuatilia Yardy na kumuona kama kielelezo.
Je, Yardy alikosea kwa kutengeneza sketi hii, au ni
sehemu tu ya burudani ya mitandao? Tupe maoni yako!