
Mbunge wa Kiharu mheshimiwa Ndindi Nyoro ambaye ni
mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika
bunge la taifa .
Ndindi Nyoro ni msomi aliyefuzu kwa shahada ya Uchumi
kutoka chuo kikuu cha Kenyatta na kwa muda uliopita alirodheshwa na mashirika mbalimbali
ya utafiti kama kiongozi mpevu na mchapa kazi.
Katika sherehe za Hamsini na tisa( 59) za kusherehekea siku
ya Jamhuri Rais William Ruto aliwahi kumtuza kama kiongozi mpachapazi kwa kuendeleza
maendeleo katika eneobunge lake la Kiharu.
Nyoro alikuwa akishikilia nafasi ya uenyekiti wa bajeti katika
bunge la taifa tangu serikali ya Kenya Kwanza ilipochukua hatamu za uongozi na
amekuwa kipenzi cha wengi kwa kuonyesha uzingativu wa hali ya juu kazini.
Kwa siku chache zilizopita bwana Nyoro amekuwa kimya tofauti
na alivyokuwa mtetezi sugu wa bwana Ruto,hata inakumbukwa wengi walisawiri
ushirikiano wa Rais Ruto na Nyoro kama
ulikuwa ni mwiba hatari kwa aliyekuwa naibu wa Rais enzi hizo Rigathi Gachagua.
Kulingana na mawimbi ya mageuzi mbalimbali yaliyotendeka
katika kamati za bunge yaliyomlenga mwenyekiti wa kamati ya bajeti bwana Nyoro na kuweza kumwondoa ili
nafasi yake ijazwe na mwenyekiti mwingine.
Katika hoja zilizotolewa na wabunge mbalimbali ili kuweza kujadili
na kupiga msasa utendakazi wa bwana Nyoro katika kamati yake ya bajeti kama
mwenyekiti viongozi mbalimbali waliweza kumkashifu kwa matumizi mabaya ya afisi.
Kiuongozi wa waliowengi bungeni pia ambaye ni mbunge wa Kikuyu
bwana Kimani Ichungwa aliweza kumkashifu bwana Nyoro kwa kujilimbikizia Madaraka
tele kwa kutenga bajeti ambayo haioani na bajeti ya fedha zilizotengwa kwa
ajili ya maeobunge yote wakilishi katika bunge la Taifa.
Vilevile Kiongozi wa walio wachache katika Bunge la Taifa Junnet
Mohammed aliweza pia kumshutumu mwana Nyoro kwa kuwa mbinafsi na mwenye kujijali
alipojitengenezea bajeti ya hela nyingi kwa ajili ya eneo bunge lake katika
kile ambacho kilitajwa kama kutokuwa na usawa kwa kutekeleza wajibu wake
ipasavyo kama mwenyekiti wa bajeti.
Kulingana na mujibu wa bwana Ichunhwa na Junet eneobunge la
Kiharu lilipokea mgao wa fedha nyingi za bajeti na za kimaendeleo kushinda
maeneobunge yoyote 289 kuashiria upendeleo na ukiukaji mkubwa wa Katiba.