Hakukuwa na dosari katika katika KCSE 2022- Waziri Machogu

Machogu alisema usimamizi wa KCSE 2022 ulikuwa safi.

Muhtasari

•Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu amesema hakukuwa na dosari katika Mtihani wa KCSE 2022.

•Mwaka jana, watahiniwa 884,263 walifanya mtihani wa Cheti cha Elimu ya Sekondari cha Kenya (KCSE)

wakati wa kuachiwa kwa matokeo ya KCSE katika Jumba la Mitihani huko Kilimani, Nairobi mnamo Januari 20, 2023.
Waziri wa elimu Ezekiel Machogu wakati wa kuachiwa kwa matokeo ya KCSE katika Jumba la Mitihani huko Kilimani, Nairobi mnamo Januari 20, 2023.
Image: ANDREW KASUKU

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu amesema hakukuwa na dosari katika Mtihani wa KCSE 2022.

Machogu alisema usimamizi wa KCSE 2022 ulikuwa safi.

Waziri huyo alisema Wizara ya Elimu ilibuni mbinu mbalimbali za kukomesha udanganyifu

"Tulikuja na utaratibu kwamba uwajibikaji ulihamishwa hadi ngazi ya mtu binafsi," Machogu alisema.

"Tulisema meneja wa kituo atawajibika binafsi kwa makosa yoyote. Tulitengeneza fomu kwa ajili ya maafisa wa usalama kuandika jinsi mambo yalivyokwenda."

Machogu alizungumza Ijumaa wakati wa kutolewa kwa matokeo ya KCSE 2022 katika jumba la Milimani house, Kilimani.

Mwaka jana, watahiniwa 884,263 walifanya mtihani wa Cheti cha Elimu ya Sekondari cha Kenya (KCSE)

Watahiniwa wa kiume walikuwa 405,962 huku wanawake wakiwa 420,845