"Kaende kaende!" Kawira Mwangaza atangaza huku akirejea kazini, atuma ujumbe kwa maadui

Alhamisi asubuhi, gavana huyo wa tatu wa Meru alidokeza kurudi kwake kazini kwa kuchapisha picha yake akiwa afisini.

Muhtasari

•Gavana huyo wa muhula wa kwanza alijifariji tena kwa fundisho la Biblia linalozungumza kuhusu Mungu kusaidia kuaibisha adui.

•“Kabati kabati kaende kaende,” alisema chini ya picha yake akiwa ofisini.

Image: FACEBBOOK// KAWIRA MWANGAZA

Gavana wa kaunti ya Meru aliyekumbwa na matatizo si haba ,Kawira Mwangaza, ameendelea kusherehekea baada ya mahakama kuu kupiga breki kubanduliwa kwake siku ya Jumatano mchana.

Alhamisi asubuhi, gavana huyo wa muhula wa kwanza alijifariji tena kwa fundisho la Biblia linalozungumza kuhusu Mungu kusaidia kuaibisha adui.

Katika chapisho lake kwenye mitandao ya kijamii, Kawira alizungumzia jinsi imani katika Mungu inavyosaidia katika kutawanya mipango ya maadui.

"Imani yako ina kile kinachohitajika kutawanya chochote ambacho adui hupanga dhidi yako!

Habari za asubuhi na zaidi Neema na Imani,” Kawira alisema.

Haya yalikariri ujumbe wake wa Jumatano baada ya mahakama kuu kumpa afueni ya muda, kufuatia hatua ya seneti kuidhinisha kubanduliwa kwake usiku wa kuamkia leo.

“Mungu mwenye rehema,” alisema kwenye Facebook.

Siku ya Alhamisi asubuhi, gavana huyo wa tatu wa Meru alidokeza kurudi kwake kazini kwa kuchapisha picha yake akiwa afisini.

“Kabati kabati kaende kaende,” alisema chini ya picha yake akiwa ofisini.

Kawira Mwangaza alionekana mwenye furaha siku ya Jumatano kutokana na uamuzi wa Mahakama Kuu kupiga breki uamuzi wa Seneti wa kuidhinisha kuondolewa kwake mashtaka.

Jaji Bahati Mwamuye wakati uo huo alimzuia Spika wa Seneti Amason Kingi kuchapisha Notisi ya Gazeti la Kenya tangazo la nafasi wazi katika afisi ya Gavana wa Kaunti ya Meru.

Mwangaza alielekea mahakamani baada ya seneti kuunga mkono kutimuliwa kwake usiku wa kuamkia Jumatano.

Maseneta 26 walipiga kura kuunga mkono shtaka la kwanza la ukiukaji mkubwa wa katiba na sheria zingine.

Maseneta 14 walikosa kupiga kura huku wanne wakipiga kura kumuunga mkono.

Katika shtaka la pili la utovu wa nidhamu uliokithiri, maseneta 26 walipiga kura ya kuunga mkono kushtakiwa kwake, wawili walipinga, huku wengine 14 wakikosa kupiga kura.

Maseneta 27 waliunga mkono shtaka la matumizi mabaya ya afisi, kura moja ya kumuunga mkono na 14 hawakupiga kura.

Wengi wa waliokosa kupiga kura ni washirika wa vyama vya Upinzani.

“Kulingana na Kifungu cha 181 cha Katiba, Kifungu cha 33 cha Sheria ya Serikali ya Kaunti na Kanuni ya Kudumu ya 86 ya Kanuni za Kudumu za Seneti, Seneti imeazimia kumuondoa afisini kwa kumwondoa madarakani Mhe. Kawira Mwangaza, Gavana wa Kaunti ya Meru na gavana huyo kukoma ipasavyo. kushika wadhifa huo," Spika Amason Kingi alisema.

Hii ilikuwa ni mara ya tatu kwa Mwangaza kung'olewa madarakanina  kufikishwa katika seneti, tangu alipochaguliwa kuwa wadhifa wake Agosti 2022.