Mdomo wake ulijazwa jozi 3 za soksi- Uchunguzi wa maiti wafichua kilichomuua Chiloba

Oduor alizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Moi baada ya zoezi lililochukua zaidi ya saa tatu

Muhtasari
  • Dkt Oduor alisema Chiloba alikufa kwa kuzibwa mdomo na pua, hali ambayo  ilisababisha yeye kukosa oksijeni.
  • Alisema wakati wa kifo hicho marehemu alikuwa hapati oksijeni ya kutosha kwenye ubongo wake ambao ulikuwa umevimba
MWANAHARAKATI EDWIN CHILOBA
Image: HISANI

Edwin Kiprotich kiptoo almaarufu Chiloba alikufa kwa kuzibwa mdomo na pua, hali ambayo  ilisababisha yeye kukosa oksijeni.

Mwanapatholojia mkuu wa serikali Dkt Johansen Oduor amesema alikufa kwa kufunikwa pua na mdomo ili kukosa hewa.

Dkt Oduor alisema alibaini mwili huo ulikuwa umeoza lakini wakati wa zoezi hilo waligundua vipande vya nguo na soksi zilizojaa mdomoni.

Dkt Oduor alisema walipata jozi tatu za soksi zikiwa zimejazwa mdomoni mwa marehemu.

Alisema wakati wa kifo hicho marehemu alikuwa hapati oksijeni ya kutosha kwenye ubongo wake ambao ulikuwa umevimba

Majeraha mengine pia yalipatikana mdomoni

Oduor alizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Moi baada ya zoezi lililochukua zaidi ya saa tatu

Alikuwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo Dk Wilson Aruasa.

Dkt Oduor alisema walikuwa wamechukua sampuli kutoka kwa mwili huo kwa uchunguzi zaidi katika duka la kemia la serikali.