Mkurugenzi wa makao ya watoto afungwa miaka 100 jela kwa kunajisi watoto wanne

Nzuki aliomba kuachiliwa na hukumu isiyo ya kutomzuilia ambayo ilikataliwa na mahakama.

Muhtasari

•Zainab alisema kutoa hukumu isiyo ya kizuizini katika kesi kama hiyo ni sawa na kukejeli mfumo wa haki.

•Mahakama katika kumhukumu Nzuki ilizingatia jinsi watoto hao ambao sasa ni watu wazima wameathiriwa na vitendo vya mshtakiwa.

Mahakama
Mahakama

Mkurugenzi wa zamani wa makao ya watoto amehukumiwa kifungo cha miaka 100 jela kwa kunajisi watoto wanne waliokabidhiwa uangalizi wake.

Hakimu Mkuu Mwandamizi Zainab Abdul alisema Stephen Nzuki alipaswa kuwalinda watoto hao  lakini badala yake akawadhulumu kwa kuwanajisi mara kwa mara.

"Kosa lililotendwa ni makuu sana na yana adhabu kubwa. Hivyo basi, ni wajibu wa mahakama hii kutoa adhabu ya kuwazuia wahalifu wengine."

Nzuki alikuwa ameomba kuachiliwa na hukumu ya kutomzuilia ambayo ilikataliwa na mahakama.

Zainab alisema kutoa hukumu isiyo ya kizuizini katika kesi kama hiyo itakuwa sawa na kukejeli mfumo wa haki.

Mahakama katika kumhukumu Nzuki ilizingatia jinsi watoto hao ambao sasa ni watu wazima wameathiriwa na vitendo vya mshtakiwa.

Katika tukio moja ambapo mtoto mmoja alikuwa na umri wa miaka tisa wakati wa kosa hilo, mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka 50.

Atatumikia miaka 20 kwa kumnajisi mtoto mwingine wa miaka 15 na miaka 20 kwa kumnajisi mtoto wa miaka 13.

Pia alipatikana na hatia ya kosa la kufanya kitendo kichafu na mtoto mdogo. Atatumikia miaka 10 kwa hiyo.

Makosa hayo yalitekelezwa kati ya 2010 na 2016 katika nyumba ya watoto ya Screams Africa iliyoko Mihango ndani ya eneo la Utawala.