Njaa yasababisha zaidi ya wanafunzi 200 wa shule ya msingi ya Juja kuacha shule

Wanafunzi wengi wanaangaliwa na babu na nyanya zao kwani wazazi wao walifariki, au wametelekeza majukumu yao.

Muhtasari

•Mwalimu mkuu alisema wanafunzi wao wengi wanatoka katika familia hohehahe ambazo haziwezi kumudu chakula.

•Eneo hilo, ambalo lina machimbo kadhaa, linajulikana kwa matumizi mengi ya pombe haramu.

ambapo zaidi ya wanafunzi 200 wameacha shule kutokana na nja
George Mimi, mwalimu mkuu, shule ya msingi ya Nyacaba huko Juja ambapo zaidi ya wanafunzi 200 wameacha shule kutokana na nja
Image: Muoki Charles

Huku njaa ikiendelea kukumba familia nyingi kote nchini, shule moja katika Kaunti Ndogo ya Juja imeathirika sana huku zaidi ya wanafunzi 200 wakiacha shule kutokana na njaa.

George Mimi, mwalimu mkuu wa shule ya Msingi ya Nyacaba, ambayo ina wanafunzi zaidi ya 1,900 

Alisema wengi wa wanafunzi hao wanaishi chini ya uangalizi wa babu na nyanya wao kwani wazazi wao walifariki, au wametelekeza majukumu yao kutokana na ulevi na hivyo kuwafanya washindwe kumudu chakula.

Alisema hali hiyo imewafanya wanafunzi kukosa masomo na kwamba ushuhuda wa wanafunzi kuhusu hali ya nyumbani kwao umekuwa wa kuvunja moyo.

"Hali katika shule hii inahitaji kuangaliwa kwa umakini. Wanafunzi wengi tulio nao wanaishi na babu na nyanya zao ambao hawana uwezo wa kuwatunza. Kutokana na kufunguka kwao, ni nadra sana kumudu kula milo miwili. Viwango vyao vya umakini na utendakazi viko chini na vinahitaji uingiliaji kati,” alisema Mimi.

Eneo hilo, ambalo lina machimbo kadhaa, linajulikana kwa matumizi mengi ya pombe haramu.

Mimi alipendekeza kuanzishwa kwa mpango endelevu wa lishe katika shule iliyo mashinani ili kuwaweka wanafunzi madarasani.

Hali hiyo ya kutisha imewafanya viongozi wa eneo hilo wakiongozwa na mbunge mteule Trizah Wanjiru kuanzisha mpango wa kutoa chakula katika shule hiyo iliyoko katika eneo la uchimbaji madini nusu kame.

Wanjiru, ambaye aliandamana na Mwakilishi wa Wanawake wa Kiambu Anne Wamuratha alisambaza chakula cha msaada kwa wakazi hao wenye njaa akisema wananuia kubuni mpango wa kulisha shuleni.

Mbunge huyo aliyezaliwa na kukulia katika kijiji hicho aliapa kukusanya rasilimali ili kuhakikisha wanafunzi wanashiba vizuri ili waendelee na masomo bila kuingiliwa.

Kwa upande wake, Wamuratha alitoa wito kwa serikali na watu wema kuendelea kusambaza chakula cha msaada katika Kaunti ya Kiambu akisema wengi wa wakazi wake wana njaa.

“Wale wanaosema kuwa Kaunti ya Kiambu ni tajiri na yenye utajiri mkubwa wa rasilimali hawapati. Tunateseka kama kaunti zingine na watu wetu wameathirika sawa na wanahitaji chakula cha msaada,” alisema Wamuratha.

Alisema wakati serikali imejaribu kusambaza chakula cha msaada, suluhu za kudumu za uhakika wa chakula zinahitajika ili kuifanya nchi kuwa endelevu hata pale mvua zinaponyesha au kuchelewa.

Alipendekeza kilimo cha umwagiliaji maji kwa kuchimba visima vya maji na mabwawa kote nchini ili kuwezesha uzalishaji wa chakula cha kutosha.

Utafsiri: Samuel Maina