Unyama! Mvulana wa miaka 3 alawitiwa na kuuawa Dandora

Muhtasari

•Mvulana huyo alipatikana amefariki ndani ya nyumba yao ambako mamake alikuwa amemuacha pekee yake na kutoka kidogo.

crime scene
crime scene

Familia moja katika mtaa wa Dandora, kaunti ya Nairobi inamuomboleza mtoto wao wa miaka mitatu ambaye alilawitiwa kisha kuuawa.

Mvulana huyo alipatikana amefariki ndani ya nyumba yao ambako mamake alikuwa amemuacha pekee yake na kutoka kidogo.

Mtoto huyo aligunduliwa kuwa amefarika muda mfupi baada ya mamake kuondoka.

Polisi walioshughulikia eneo la tukio walisema mwili wa mvulana huyo ulikuwa umelazwa kitandani huku damu ikivuja kutoka mdomoni, puani na sehemu ya haja kubwa.

Mkuu wa polisi katika eneo la Buruburu Kamau Ngugi alisema uso wa mvulana huyo ulikuwa umevimba, jambo linaloashiria kuwa alipigwa.

Ngugi alisema wapelelezi wa eneo la uhalifu la waligundua kitanda hicho kilikuwa kimefurika maji na pia walipata pakiti tupu ya kondomu.

Utata mkubwa umezingira kisa hicho na polisi bado hawajaweza kubaini kilichopelekea tukio hilo. Wameeleza kuwa wanakusudia kufanya uchunguzi wa maiti.

"Hakuna aliyekamatwa hadi sasa lakini timu zetu zinashughulikia suala hilo," mkuu wa polisi alisema.