Hafla ya mazishi ya Tob Cohen yatangazwa. Watakaohudhuria watajwa

unnamed (1)
unnamed (1)
Hatimaye taarifa imetolewa kwamba mwili wa marehemu Tob unatarajiwa kuzikwa jumatatu wiki ijayo.

Mawakili kutoka pande zote za familia wamefikia uamuzi wa kwamba Cohen azikwe katika makaburi ya Kiyahudi jijini Nairobi.

Soma hadithi nyingine;

Mazishi haya yanatarajiwa kufanyika saa nane alasiri.

Mila na itikadi za wayahudi zinasema kuwa mwili wa mwendazake unafaa uzikwe baada ya masaa 36.

Kanuni hizi hazingefuatwa ukizingatia msururu wa matukio yanayotokea.

Soma hadithi nyingine;

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi, Cliff Ombeta akiwa na Philip Murgor wametangaza kuwa mjane wa Cohen Sarah na dadake Tob watakuwepo katika hafla ya mazishi.

'Itikadi za mazishi zitakwenda sawa na mila za wayahudi na zitaendeshwa na viongozi wanaohusika wa jamii hiyo" Amesema Ombeta.

Kwa mujibu wa Murgor na Cliff, DPP,DCI na viongozi wa idara ya mahakama wameombwa na Sarah na Gabrielle kuendesha hafla hiyo.

Mwili wa bilionea huyu ulipatikana wiki iliyopita Ijumaa baada ya kupotea kwa wiki 8.

Soma hadithi nyingine;

 Mwili huu uliokuwa umeanza kuoza ulipatikana Ijumaa alasiri .

Ulikuwa umefungwa mara kadhaa ndani ya mifuko ya plastiki. Cohen aliripotiwa kutoweka kutoka boma lake la Lower Kabete jijini Nairobi mnamo Julai 19 na 20.