Hafla za tohara lazima zifuate masharti ya afya kuhusu covid-19 - Kagwe

Hafla za tohara zinazoendelea katika maeneo mbali mbali ya magharibi mwa nchi lazima zifuate kanuni zilizowekwa na wizara ya afya nchini, waziri wa Afya Mutahi kagwe amesema.

Waziri Kagwe alisema kwamba anafahamu tamaduni ya tohara inayoendelea katika maeneo ya Magharibi lakini aliwashauri wenyeji kuzingatia sana kauni za afya ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Soma habari zaidi:

"Tunataka kuhakikisha kuwa hakuna hafla ya tohara itakayofanywa bila kufuata masharti yaliowekwa kuokoa kila mtu," Kagwe alisema.

Jamii ya waluhya kutoka magharibi mwa Kenya huendesha zoezi la kutahiri wavulana kila baada ya miaka miwili mwezi wa Agosti,  na huu ni mwaka wa zoezi hilo.

Soma habari zaidi:

Licha ya wataalam wa afya kushauri wananchi wa eneo hilo kutoendesha zoezi hilo mwaka huu kutoka na hatari za maambukizi ya virusi vya corona baadhi ya familia zimepuuza ushauri huo na zinaendelea na zoezi hilo.

Kenya siku ya Jumamosi ilisajili jumla ya visa 699 vya maambukizi mapya ya covid-19 huku watu 781 wakipona ugonjwa huo chini ya saa 24.