'Haikuwa pesa za wizi, alinizawidi baada ya kula uroda,' mjakazi ajitetea

Ruth Khaecha
Ruth Khaecha
'Haikuwa pesa za uwizi, alinituza baada ya kula uroda," Hivyo ndiyo alivyojibu mjakazi Ruth Khaecha baada ya kukana madai ya kuiba shilingi 1,350,000 kutoka kwa mwajiri wake wa zamani Paul Mwangi.

Aidha, Khaecha alisema kwamba alipewa shilingi 800,000 kama zawadi baada ya kumpa 'mapenzi matamu.'

Hivyo ndivyo  alivyotoa ushahidi kortini Januari 15.

Lakini baada ya hakimu Heston Nyaga wa mahakama ya Makadara aliposikiza kesi hiyo tena Ijumaa, Khaecha alipatikana na hatia ya kumuibia mwajiri wake pesa na akahukumiwa kifungo cha miaka 3 gerezani.

Korti iliamuru kuwa shamba alilonunuliwa kwa kitita cha shilingi 570,000 liuzwe ili pesa zirejeshewe mwenyewe.
Aidha shilingi 500,000 na nyingine 70,000 ambazo mshukiwa alikuwa amempa baba yake zilipatikana katika begi lake.
Hata hivyo, wakati kesi hiyo ikiskizwa mshtakiwa alisema kwamba 'alitekeleza wajibu wake vyema kitandani.'

Kisha akasema kortini kwamba baada ya kitendo hicho Mwangi alimpa bahasha.

Khaecha aliambia mahakama kuwa aliamua kugura eneo hilo kwa kuwa mkewe, Jane Wairimu alikuwa anashuku kutokana na 'jinsi alivyokuwa akimpigia kelele.'

Aidha alisema kwamba alifanya kazi kwa miezi miwili unusu huku mshahara wake ukiwa shilingi 6,500 kila mwezi.

Mwangi alithibitishia korti kwamba mshtakiwa alilipa hizo pesa na kutoroka bila maagano rasmi.

"Nilipofika nyumbani, nilipata nyumba ikiwa imefungwa, na mshtakiwa hakuwa. Nilijaribu kumpigia simu lakini sikufaulu." alisema