Hakuna mganga wa kumsaidia Kiraitu uchaguzini-Aburi

Hakuna mganga wa kumsaidia Kiraitu uchaguzini-Aburi

Mbunge wa  Tigania East  Mpuri Aburi  na seneta wa Meru  Kiraitu Murungi  wamekanusha  madai kwamba  watamtumia mganga  kuhakikisha kwamba  Kiraitu anashinda kiti cha ugavana katika uchaguzi wa mwaka huu .

Wakizungumza katika hafla tofauti wawili hao wamevishtumu vyombo vya habari kwa  kuongeza chumvi utani uliotolewa na  bwana James Mugambi Barongo al maarufu  ‘Kaana Ka Njoka’ aliyesema ana  nguvu za kiganga kumsaidia kiraitu kushinda kiti hicho .

Mugambi aliwatishia wale ambao hawatompigia kiraitu kura kwamba wataaga dunia. Lakini sasa wamejitenga na vitisho hivyo na kuviita ‘utani’ wa  ‘kuwachekesha  watu’ .