Hakuna Njama ya Kumwua Naibu wa Rais Ruto-Munya

   Mawaziri wanne  walioagizwa  kufika mbele  katika makao makuu  ya DCI wamepuuza madai ya kuwepo  njama ya kumwua naibu wa rais  William Ruto .waziri wa viwanda Peter Munya  amesema maafisa hao hawakuwa na  taarifa ya malalamishi kutoka kwa Ruto .Amesema wako tayari kurejea kwa DCI ili kujibu maswali yoyote .

Mkusanyiko wa Habari na Matukio Muhimu Tarehe 24 Juni 2019

Jaza fomu za kodi kabla ya makataa 

Una siku sita zilizosalia ili ujaze fomu za kuthibitisha kwamba umelipa kodi mwaka uliopita . wale wasio na mapato wanatakiwa kujaza fomu hizo kuonyesha kwamba hawakulipa kodi chochot kama kodi .

 Jaji Mkuu kuunda jopo la kusikiza kesi  za kupinga marupurupu ya wabunge

Kesi mbili zinazolenga kuwazuia wabunge kupokea marupurupu  ya nyumba zimehamishwa hadi kwa jaji mkuu    ili aunde jopo la majaji wa kuzisikiliza .  mwanaharakati Okiya Omtatah  na tume ya SRC wanataka wabunge kuzuiwa kupokea shilingi elfu 250 kila mmoja kama  marupurupu ya nyumba  na kurejesha fedha  walizopewa .

Watahiniwa wa KCPE kuchagua shule wanazotka kujiunga nazo

Watahiniwa wanaofanya mtihani wa KCPE   mwaka huu  wana hadi mwisho wa mwezi ujao  kutathmini upya shule za upili wanazotaka kujiunga nazo mwezi januari .  mtindo huo ni mpya kwani kwa kawaida watahiniwa huzichagua shule za upili baada ya  matokeo kutolewa .  katibu wa kudumu wa elimu Belio Kipsang amesema hatua hiyo itapunguza muda  unaotumiwa katika utaratibu wa  usajili wa kidato cha kwanza .

  Zoezi la kuwaajiri majaji laingia  wiki ya pili

Shughuli ya  kuwaajiri majaji wa mahakama ya rufaa  imeingia wiki ya pili leo  huku  watu wanne  wakitarajiwa kuhojiwa leo .wanne hao ni  majaji  Hedwig Ong’udi, Hellen Omondi, Joseph Sergon  na  Nixon Sifuna.  Jopo linaloongozwa na Jaji mkuu David Maraga  linatarajiwa kuwahoji watu 33 waliotuma maombi ya kupewa kazi hizo kufikia julai tarehe mosi .

 Ugonjwa wa kipindupindu unaweza kutibiwa 

Wagonjwa walio na daalili za ugonjwa kipindupindu  wanaweza kupona endapo watatipiwa mara moja . mtaalm wa afya ya umma Josephine Odanga  amesema mgonjwa wa kipindu pindu anafaa kukimbizwa kwa kituo cha matibabu haraka iwezekanavyo ili kuongezwa maji mwilini .